Mwathirika asimulia walivyoteswa na polisi Nigeria

0

LAGOS,NIGERIA

SHAHIDI wa kwanza katika uchunguzi wa Nigeria kuhusu ukatili wa polisi ameelezea jinsi alivyoteswa na kung’olewa meno na maafisa wa kikosi maalum cha polisi wa kupambana na ujambazi (Sars).

Okoye Agu alikamatwa baada ya mkubwa wake kumtuhumu kwa wizi kazini.Jopo la uchunguzi katika jimbo la Lagos lilibuniwa kufuatia maandamano ya nchi nzima kushinikiza Sars ivunjiliwe mbali.

Huenda pia likachunguza kisa cha watu kupigwa risasi katika maandamano ya wiki iliyopita ambapo makundi ya kutetea haki yalisema watu 12 waliuawa.

Katika ushahidi, Agu alielezea jinsi mwaka 2014 alivyopigwa na kutambulishwa kwa umma kama mhalifu, kisha akaning’inizwa kichwa chini miguu juu na kung’olewa meno mawili.

Pia aliongeze kuwa gari lake na simu zake za rununu ziliuzwa na maafisa wa Sars bila idhini yake.Polisi wamekataa kumlipa faidia licha ya agizo lililotolewa na mahakama, aliaambia jopo hilo linaloongozwa na jaji mstaafu.

Alisema familia yake haikujua alikuwa wapi walipompata katika kituo cha polisi baada ya kumtafuta kwa siku 47, mke wake na mama yake pia walipigwa mbele yake.

Ushahidi wa Agu ulishabihiana na matamshi yaliotolewadhidi ya maafisa wa Sars, ambao wamesemekana kuwanyanyasa, kuwapiga na wakati mwingine kuwaua watu.

Kesi zingine zilizokuwa zimepangwa kusikizwa Jumanne ziliahirishwa baada ya kukosekana kwa mashahidi muhimu.

Mauaji hayo yanayodaiwa kutekelezwa na kitengo maalum cha polisi kinachochukiwa yalizua maandamano kote nchini Nigeria yaliyopangwa chini ya hashtag ya #EndSars. Waandamanaji walimlazimisha Rais Muhammadu Buhari kukivunja kitengo hicho.

Kufanyika kwa uchunguzi huru dhidi ya ukatili wa polisi ndio matakwa makuu yaliyoshinikizwa na waandamanaji kote nchini kwa zaidi ya wiki mbili.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari

Serikali kuu imetoa maelekezo kwa mamlaka za majimbo 36 kubuni tume ya uchunguzi na usikilizwaji wa Jumanne ulikuwa wa kwanza nchini.

Jopo hilo la wanachama 11, miongoni mwa wawakilishi wa waandamanaji, kwa kipindi cha miezi sita ijayo ambapo litasikiliza na kunakili ushahidi wa waathiriwa wote ama kuzungumza na familia za wahanga wa ukatili wa Sars.

Pia litatoa mapendekezo ya jinsi waathirika watalipwa fidia kwa njia gani pamoja ia kutathmini ikiwa maafisa waliohusika wanastahili kufunguliwa mashtaka.

Jopo pia litatoa  mapendekezo ya jinsi ya kuhakikisha ukatili kama huo unakomshwa Gavana wa Lagos, Babajide Sanwo-Olu ametangaza kuwa uchunguzi umepanuliwa ili kujumuisha visa vya ghasia katika lango la Lekki Oktoba 20 ambapo mashuhuda na mashirika ya kutetea haki Amnesty International yalisema wanajeshi waliwapiga risasi waandamanaji na kuwaua baadhi yao.

Jeshi limekana kuhusika na mauaji hayo

Watu watakuwa wakifuatilia kwa karibu uchunguzi huo kuona ikiwa serikali itatekeleza mapendekezo yatakayotolewa na jopo punde litakapokamilisha kazi yake kwasababu kumekuwa na historia ya muda mrefu wa mamlaka kupuuza matokeo ya uchunguzi wa asasi kama hizo, anasema mwandishi wa BBC Nduka Orjinmo akiwa mji mkuu wa Abuja.

Kwa mfano mamlaka haijawahi kutekeleza mapendekeza yaliyotolewa kuhusu uchunguzi wa mauaji ya zaidi ya Washi 300 yaliyofanywa na majeshi ya Nigeria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here