Home BURUDANI Mwanamuziki Manu Dibango amefariki kwa ugonjwa wa corona

Mwanamuziki Manu Dibango amefariki kwa ugonjwa wa corona

NA MWANDISHI WETU

Mwanamuziki, mwandishi na mpuliza saxophone, raia wa Cameroon Duniani Emanuel N’djoke Dibango maarufu Manu Dibango amefariki dunia kwa Ugonjwa wa Virusi vya Corona leo machi 24, 2020.

Kutoka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook taarifa za kifo chake ziliandikwa “Ni machungu na huzuni kubwa kutangaza kwamba Dibango amefariki leo 24 -3-2020 akiwa na umri wa miaka 86,”.

Moja kati ya visa vya kukumbukwa ni pale marehemu Manu Dibango alipodai hakimiliki kutoka kwa gwiji wa Pop duniani Michael Jackson kwa kutumia vionjo vya Soul Makossa ya Dibango katika wimbo wa Wanna Be Startin’ Somethin’ wa Michael Jackson.

Dibango alitamba sana katika upulizaji saxophone, muziki wa Jazz, uandishi wa nyimbo na hata kuchanganya vionjo vya asili toka Cameroon na kuvipaza katika majukwaa ya kimataifa Duniani.

Dibango ameacha watoto watatu, Georgia Dibango, Marva Dibango, Michael Dibango.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments