Mwanahabari aliyetangaza mlipuko wa kwanza wa virusi vya corona afungwa

0

HONG KONG,CHINA

MWANDISHI wa habari wa nchini China amefungwa kwa kuripoti mlipuko wa virusi vya corona kwa mara ya kwanza..

Zhang Zhan alipatikana na kosa la “kuanzisha uvumi na kuzua vurugu”, mashataka mara kwa mara dhidi ya wanaharakati

Wakili huyo wa zamani aliye na umri wa miaka 37 aliyezuiiwa mwezi Mei, amegoma kula kwa miezi kadhaa. Mawakili wake wanasema afya yake imedhoofika vibaya.


Zhang ni mmoja wa wanahabari kadhaa raia wa China waliojipata mashakani kwa kuripoti kuhusu mwenendo wa virusi vya corona katika eneo la Wuhan.

Hakuna vyombo huru vya habari nchini China na mmalaka inajulikana kwa kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wanaharakati wanaoonekana kuhujumu juhudi zaa serikali kukabiliana na mlipuko huo.

Zhang aalifikishwa katika mahakama ya Shanghai akiwa na wakili wake Jumatatu asubuhi.Kwa mujibu wa mashataka yanayomkabili, alisafiri hadi Wuhan mwezi Februari kuripoti kuhusu mlipuko wa virusi bila kuzingatia kanuni zilizowekwa.

Ripoti yake aliyoweka mubashara katika mtandao wa kijamii ilivuma sana mwezi Februari, ilimweka mashakani baada ya kuvutia mamlaka za China.

Mtandao wa China wa kutetea haki za binadamu ulisema ripoti zake zilijumuisha habari za kuwekwa kizuizini kwa waandishi huru wa habari na unyanyasaji wa familia za wahanga ambao walikuwa wakitafuta uwajibikaji.

Zhang alitoweka Wuhan mnamo Mei 14 kwa mujibu wa CHRD. Siku moja baadae, ilifichuliwa kwamba alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Shanghai, zaidi ya kilo mita 640 kutoka hapo.

Alishtakiwa rasmi mwezi Novemba. Nyaraka za mahakama zinasema alitoa “taarifa za uonga kupiti aujumbe mfupi, video na kupitia [mitandao kama] WeChat, Twitter na YouTube”.

Pia anatuhumiwa kwa kukubali kuhojiwa na vya vyombo vya habari vya kigeni “kueneza habari za uvumi” kuhusu virusi huko Wuhan.Kifungo cha kati ya miaka minne na mitano kilipendekezwa kutolewa dhidi yake. 

Katika hatua ya kulalamikia kukamatwa kwake, Bi Zhang amegoma kula na inasadikiwa kuwa afya yake imekuwa mbaya.

Mmoja wa mawakili wake alisema katika taarifa kwamba alipoenda kumtembelea mapema mwezi Desemba alisema atalazimishwa kula kupitia mipira.

Pia alisema kuwa anaumwa na kichwa, kuhisi kisunzi na kuumwa na tumbo.

“Kufunga kula kwa saa 24 kwa siku, anahitaji kusaidia kwenda masalani, na hapati usingizi,” Wakili wake Zhang Keke alisema. “Anapata usumbufu wa kiakili kutokana na dhiki anayopitia kila siku.”

Wakili huyo alikuwa amewasilisha mahakamani ombi la kutaka kesi dhidi ya mteja wake kuahirishwa kutokana na hali afya ya  Zhang.

Hii sio mara ya kwanza Zhang amechukuliwa hatua na mamlaka za China.

Kwa mujibu CHRD, aliagizwa kufika polisi mjini Shanghai Septemba 2019 na kuzuiliwa kwa kuunga mkono wanaharakati wa Hong Kong

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here