Mwalimu mbaroni kwa kumbaka, kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tano

0

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mwalimu wa taalumu wa shule ya msingi  Montfort iliyopo manispaa ya Morogoro,   Eneza Anderson (27) kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa  darasa la tano wa shule hiyo.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne Novemba 10,  2020  kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro,  Wilbroad Mutafungwa amesema taarifa za tukio hilo zilitolewa polisi Novemba 5,  2020 saa 6 mchana kupitia dawati la jinsia na watoto.

Kamanda Mutafungwa amesema  mwanafunzi huyo alipohojiwa alidai kuingiliwa kimwili na mwalimu wake  mara kwa mara maeneo ya ofisini na chooni wakati wanafunzi wenzake wanapokuwa darasani.

Amesema  mtuhumiwa naye alihojiwa na polisi na alikiri kumlawiti mtoto huyo wa kike mara tano hata hivyo polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.

Amesema hatua za kumfikisha mahakamani mwalimu huyo zinafanywa na polisi kwa kushirikiana na maofisa ustawi wa jamii mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Kamanda Mutafungwa amesema tayari mtoto huyo ameshafanyiwa uchunguzi na madaktari na imethibitika kuwa amebakwa na kuingiliwa kinyume cha maumbile zaidi ya mara moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here