Mvua kubwa kunyesha mikoa sita nchini, Dar yatajwa

0

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha kwa siku tatu mfululizo  kuanzia leo Jumapili Novemba 8,  2020.

Imesema athari zinazoweza kujitokeza ni mafuriko kwenye makazi ya watu, baadhi ya barabara kufungwa na shughuli za kiuchumi kusimama.

Mamlaka hiyo imesema mvua  zitanyesha mkoani Dar es Salaam, Morogoro,Tanga, visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Zinatarajiwa kuanza leo hadi Novemba 10, 2020 na  kwamba inatarajiwa maeneo hayo yatakuwa yenye tahadhali kubwa hususani  leo na kesho ambapo vipindi vikubwa vya mvua vinatarajiwa kujitokeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here