KAMPALA, Uganda
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amezindua ila yake ya uchaguzi ya miaka mitano ijayo kwa ajili ya uchaguzi Mkuu utakafaonyika nchini humo Februari, 2021.
Museveni anayegombea nafasi hiyo mara ya 34 ametaja vipaumbele vyake kuwa ni; “kuongeza ajira, kutoa elimu na huduma za afya, kuhakikisha haki na usawa, ulinzi wa mali na maisha, na kutimiza mwingiliano wa uchumi na siasa.
“Upatikanaji wa umeme, ujenzi wa barabara na reli na kuwalipa vizuri wanasayansi wa serikali.”
Museveni alianza kuongoza Taifa la Uganda mwaka 1986 kupitia chama tawala cha NRM baada ya Mapinduzi ya kijeshi.