Mugalu aweka wazi mipango yake

0

Na Mwandishi Wetu

CHRIS Mugalu mshambuliaji namba mbili ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesema kuwa anataka kufunga zaidi ya mabao 15 kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Mshambuliaji namba moja kwa sasa ni Meddie Kagere ambaye kwenye ligi amefunga mabao manne akifuatiwa na Mugalu mwenye mabao matatu ambayo alifunga kwenye mechi zake tatu za ligi mfululizo alipoingia uwanjani.

Alianza kuwafunga Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa na alifunga bao la pili wakati Simba ikishinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa na alifunga bao lake la tatu Uwanja wa Jamhuri Dodoma wakati Simba ikishinda mabao 4-0.

Mugalu alisema:”Ninapenda kufunga ndani ya uwanja na hivyo ndio kazi yangu hivyo nitafunga mabao mengi kila nikipata nafasi ndani ya uwanja na ninafurahi kufunga na nifuraha kwangu kufunga.

“Kikubwa ambacho ninafikiria kwa sasa nikuona kwamba timu yangu inashinda kwanza na mambo mengine yatafuata, nipo hapa Simba ninafurahi hivyo kwanza ninafikiria ushindi wa timu kisha mimi nitafuata na nikifunga mabao zaidi ya 15 nitafurahi,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here