Muda wangu wa kufunga bongo umewadia- Sarpong

0

NA MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong, amesema kuwa anaamini wakati wake wa kufunga mabao ndani ya timu hiyo umeshafika baada ya kutambua ugumu wa ligi ya Tanzania tofauti na alipokuwa awali.

Sarpong alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sports ya Rwanda amefunga bao moja pekee, akikabiliwa na ukame mzito wa mabao

“Nashukuru mambo yanabadilika kadiri muda unavyokwenda, sina desturi ya woga nikiwa uwanjani kwa sababu napenda kuipigania timu yangu kupata matokeo bila ya kujali nimefunga mimi au vipi licha ya mabeki kukamia.

“Kikubwa ninachokiangalia ni suala la kufunga na muda naamini umefika wa kuweza kufanya hivyo, kwa sababu sasa hivi najua ugumu wa mabeki ulikuwa wapi na vipi nitaweza kukabiliana nao katika kuhakikisha nafunga, kwa kuwa hilo ndiyo jambo kubwa ndani ya kichwa changu kwa sasa, ligi imekuwa na ugumu kutokana na wao kukamia, tofauti na sehemu niliyotoka,” alisema Sarpong.

Kwa sasa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Cedric Kaze imeweka ngome yake ndani ya kanda ya ziwa ambapo ilimalizana na KMC Uwanja wa CCM Kirumba na kushinda mabao 2-1 Oktoba 25 mwaka huu na kusepa na pointi zake tatu.

Ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi saba imeshinda sita na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Biashara United utakaochezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 30.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here