Muda wa Carlinhos kuondoka Yanga umewadia

0

CARLOS Carlinhos raia wa Angola mwenye uwezo wa kupiga mipira iliyokufa ndani ya kikosi cha Yanga huenda akatolewa kwa mkopo ama akaachwa Jumlajumla ndani ya kikosi hicho.

Habari zinaeleza kuwa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ni sababu ya nyota huyo kuwekwa kando kwa kuwa ameshaondolewa kwenye mfumo.

Muangola huyo anasumbuliwa na majeraha ya nyonga ambayo aliyapata alipokuwa mazoezini jambo.

Hakuwa kwenye kikosi kilichoshinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji na hatakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza na Ihefu jana,Desemba 23 Uwanja wa Sokoine.

Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga kuhusu suala hilo alisema kuwa kwa sasa wanajiendesha kidijidatal hivyo kila kitu kitawekwa kwenye mitandao yao.

Yanga ikiwa imetupia jumla ya mabao 25 amehusika kwenye mabao manne, amefunga mawili na ana pasi mbili za mabao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here