Mtemvu aitaka DAWASA kufikisha maji kwa wananchi kikamilifu

0

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Issa Mtemvu ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kukamilisha kazi ya kufikisha maji kwa wananchikwa kuwaunganisha na mitandao mikubwa ya maji ilikuharakisha upatikanaji wa huduma maji.

Mtemvu ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kutembeleamiradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka kwa lengo la kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi ipasavyo.  

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika kwenye kata ya Kawe, Ubungo na Kibamba, Mtemvu amesema utekelezaji wa miradi ya maji kwa maeneo yote unaendelea vizuri.

Hatahivyo, tumebaini uwepo wa changamoto mbalimbalizinazochelewesha upatikanaji wa huduma ya maji kwa Wananchi,” amesema.

Amebainsha kuwa ziara imetokana hiyo imetokana na majadiliano yaliyotokana Na kikao kazi cha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na wabunge 16 chini ya Mtendaji  Mkuu wa DAWASA.

Mtemvu amesema kuwa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo aliyotembelea, hususanikata ya Kibamba.

Tumebaini kuna kazi ndogo iliyobaki ya kukamilisha maunganisho ya maji toka kwenye mtandao mkuu wa maji kwenda  kwa wananchi na hivyo kuchelewesha upatikanaji wa maji kwa wananchi,” ameeleza.

Tunatambua kuwa ipo nia njema kwa DAWASA kuanzia kwa Mtendaji Mkuu na Mameneja wote ya kutatua changamoto za maji, tunaamini kazi iliyobaki ya kukamilisha maunganisho ya mabomba toka kwenye mtandao mkuu kwenda kwenye nyumba za wananchi itakamilika na wananchi watapata maji kikamilifu,” amesema.


Amesema
 ipo kazi kubwa inayofanyika ya utekelezaji wa miradi mikubwa inayoenda kumaliza changamoto ya maji kwa Kata za Kibamba, Ubungo na Kawe.

Tunaimani kubwa na watendaji wa Mamlaka kwamba wataenda kufanya kazi ya kutatua changamoto zilizoonekanakwenye maeneo yaliyopitiwa,” amesema Mbunge. 

Mtemvu amesema ziara hiyo imemfanya ajifunze namna DAWASA inavyoitahidi kushughulikia tatizo la upatikanaji wamaji kwenye sehemu korofi kwa kutumia njia ya mbadala na yaharaka.  

Kwa upande wake Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Ubungo, Gilbert Masawe amesema Mamlaka imejipanga kuhakikisha  inafikisha huduma ya maji wa wananchi husika.

Kwa sasa mpango uliopo ni ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji eneo la mshikamano litakalo hudumia wakazi wa maeneo ya Msakuzi yasiyokuwa na mtandao.

Mamlaka inaendelea na zoezi la kufanya tathmini ya uwezo wamsukumo wa maji kwenye eneo la Mbezi makabe kwa lengo la kufikisha maji kwa wakazi wote wa maeneo hayo,” amesema.

Meneja wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Kibamba, Elizabeth Sankere amesema  Mamlaka inatekeleza mradi wa kulaza mabomba  kwenye eneo la urefu wa kilomita 1.5 kwa lengo la kuwafikishia huduma ya maji wakazi wa hondogo mungumwema.

Mpaka sasa mkandarasi ameshaanza kazi ya kushughulikia mtandao wa mabomba ya maji na kazi inaendelea kwa ushirikiano   na wananchi.

Diwani kata ya Msigani, Hassan Mosha aliwataka wananchi wa Kata hiyo kuwa na imani na Mamlaka na wategemee mabadiliko makubwa kwa sababu imeweka viongozi wapya kwenye maeneo yao wenye uwezo wa kutatuachangamoto ya maji kwa ufanisi mkubwa.

“Nina imani kubwa kuwa DAWASA inayotekeleza miradimikubwa ya maji, hawatashindwa kutatua changamoto yaupatikanaji wa maji kwenye maeneo haya, na kwa kuwa nimitaa mitaa michache yenye changamoto ya upatikanaji wa majikwenye Kata hii,” ameeleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here