Msuya amuombea kura Magufuli, amtabiria ushindi

0

Na Mwandishi Wetu 

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Cleopa Msuya amesema kwake yeye mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli ni mtu mwema na anastahili kuwa Kiongozi Kwani kupitia kwake Watanzania wanapata maendeleo.

Msuya ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 21, 2020 wakati akimuombea kura Magufuli katika Mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Cleopa Msuya uliopo Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Msuya amesema; Nakutakia kheri katika kampeni hii  na wana- Mwanga kwa hakika wataungana Watanzania wengine kukupa kura zote kulingana na wingi wao, pamoja na Wabunge na Madiwani wa CCM, tuna matatizo madogo madogo na imani watayashughulikia hao.”

“Kuna vijana wananiuliza utamkumbukaje Mhe. Magufuli?, ningeulizwa kwa kifupi ningesema ni mtu ambaye ambaye ameshika funguo kila mahali Ili watu wajitafutie na wapate riziki zao,” alisema Msuya.

Aidha naye Dk. Magufuli kwa upande wake ameeleza namna alivyopata shida wakati akiwa Waziri wa Ujenzi alipoamua kujenga barabara ya lami hadi nyumbani kwa Msuya.

“Nashukuru kwa mapokezi hapa Mwanga, huwezi kuitaja Mwanga bila kumtaja mzee Msuya, nikiwa waziri wa Ujenzi nilisimamia ujenzi wa barabara ya kwenda kwake, watu walihoji sana lakini historia yake kwenye taifa hili ni kubwa” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here