Mshirika mkuu wa Trump ampongeza Biden

0

NEWYORK,MAREKANI

AFISA wa ngazi ya juu wa chama cha Republican cha Donald Trump, na kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti nchini Marekani-Mitch McConnell, amempongeza Joe Biden kwa ushindi wake katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita.

Senata McConnell alizungumza baada ya wajumbe wa uchaguzi -electoral college kuidhinisha rasmi ushindi wa  Biden dhidi ya Trump.

Mdemocrat alishinda kura za wajumbe 306 dhidi ya Trump ambaye alipata kura 232.

Rais Trump bado hajakubali kushindwa, na amekuwa akiendelea kutoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa wa kura.

Mahusiano ya na bunge la Seneti ambalo kwa sasa linadhibitiwa na Warepublican, yatakuwa muhimu kwa urais wa Biden.

Alitembelea Atlanta, Georgia, kufanya kampeni kwa ajili ya Wademocrat katika uchaguzi ujao wa marudi wa seneti. Viti viwili vitaamuliwa mwezi wa Januari tarehe tano na vinaweza kuwamua iwapo chama chake kitachukua udhibiti wa bunge hilo au la.

Baada ya kuidhinishwa kwa  Biden kama rais ajaye siku ya Jumatatu, viongozi watatu wa dunia ambo awali walikataa kumpongeza rais mteule Awalifanya hivyo: Rais wa Urusi Vladimir Putin, rais wa Brazil air Bolsonaro na rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador.

Akizungumza katika bunge la Seneti , McConnell alisema kuwa anatumai kutakuwa na “matokeo tofauti ” na yale ya tarehe 3 Novemba lakini wajumbe wa uchaguzi wamezungumza .

 “Kwahiyo leo ninataka kumpongeza rais mteule Joe Biden,” alisema.

Pia alimpongeza mgombea mwenza wa Bw Biden, Kamala Harris, na kuongeza kuwa aliongeza .

“Wamarekani wite wanaweza kujivunia kuwa na makamu wa kwanza wa rais mteule mwanamke kwa mara ya kwanza kabisa .”

Biden alisema baadaye kuwa alikuwa amezungumza kwa simu na Bw McConnell kumshukuru na wawili hao walikubaliana “kukutana haraka bila kuchelewa “.

Katika mahojiano na kituo cha habari cha ABC News, Bi Harris alisema kuwa ameafiki kauli za McConnell . “Ingelikuwa vizuri kama angezitoa mapema lakini ilitokea , na hilo ndilo la muhimu . Tuendelee mbele na pale tutakapoweza kuelewana , tufanye hivyo .”

Kiongozi wa wabunge wa seneti wa chama cha Democratic Chuck Schumer alimtaka Trump ” kumaliza muhula wake kwa baraka na heshima”.

“Kwa ajili ya demokrasia, kwa ajili ya kukabidhidna madaraka kwa amani , anapaswa kuacha kutokuwa mkweli na kukubali kuwa Joe Biden atakuwa ndiye rais wetu ,” alisema.

Rais Trump haonekani kuibadilisha msimamo wake. Alituma ujumbe wa Twitter Jumanne , akisema bila kutoa ushahidi kwamba ”kuna ushahidi mkubwa wa wizi wa kura “uliomiminika “.

Akizungumza katka mkutano wa umati wa watu waliompokea alipowasili mjini Atlanta, Biden aliwashukuru wapigakura kwa kuwa na imani na “kusimama imara”, akisema :

 “Sauti yenu ilisikika , kura yenu ilihesabiwa, kuhesabiwa na kuhesabiwa tena. Ninaanza kufikiria kama nilishinda Georgia mara tatu .”

Lakini alisisitiza kwamba kuhakikisha mambo yanafanyika, anahitaji maseneta wawili wa Deocrat.

“Nitumie wanaume hawa wawili na tutaweza kudhibiti bune la seneti na tutabadili maisha ya watu wa Georgia,” Bwan Biden alisema, akiongeza kua Seneti inapaswa kuwa iliidhinisha fedha za msaada wa Covid-19 “miezi kadhaa iliyopita ” lakini haikufanya “chochote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here