Mshambuliaji Yanga, Ditram Nchimbi atimiza mwaka bila kufunga goli

0

Mshambuliaji wa Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu soka Tanzania Bara Young Africans, Ditram Nchimbi amefikisha mwaka mmoja bila kufunga goli ligi kuu ya Vodacom.

Striker huyo wa Wananchi, Ditram Nchimbi aliifungia Yanga goli lake la mwisho siku ya Jumamosi ya Februari 29 mwaka 2020 kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya klabu ya Alliance dakika ya 72 akitokea benchi kwenye ushindi wa magoli 2 – 0.

Hivyo mpaka leo hii Februari 28, 2021 ikiwa zimesalia saa chache kabla ya kuanza mwezi Machi nyota huyo anafikisha mwaka sasa pasipo kufumania nyavu Vodacom Premier League.

Ditram Nchimbi amesajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo mwaka 2019 akitokea Azam FC wakati akiitumikia kwa mkopo Polisi Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here