Morrison hatihati kuikosa Yanga kwa utovu wa nidhamu

0

NA MWANDISHI WETU

KUTOKANA na utovu wa nidhamu alionesha juzi, kiungo wa Simba, Bernard Morrison kuna hatihati akaukosa mchezo wa dabi ya Kariakoo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7 mwaka huu, dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (5)(5.2) mchezaji yeyote atayepigana au kupiga kabla ya mchezo au baada ya mchezo kumalizika basi atafungiwa michezo isiyopungua mitatu na faini isiyopungua sh. 500,00.

Pia Kanuni ya 39(6) mchezaji atayebainika kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu yanayojirudia au mara nyingi atafungiwa kucheza kati ya michezo 5 mpaka 10 na faini isiyopungua sh1m.

kutokana na kanuni hizo kama zitafuatwa kama zilivyo basi ni wazi kuwa mchezaji Morrison ataikosa Yanga kwa kuwa kanuni ya 35 inasema atafungiwa michezo 3 ambapo simba imebakisha michezo miwili ili kukutana na Yanga.

Kwenye mchezo wa Okotoba 26 uliochezwa Uwanja wa Uhuru kati ya Simba na Ruvu Shooting, Morrison alionekana akimpiga mchezaji wa Ruvu Shooting baada ya mchezo kusimama dakika ya 72 kutokana na kutokea kwa vurugu.

Vurugu hizo zilisababishwa na wachezaji wa Ruvu Shooting kugomea penalti waliyopewa Simba na ilipiga na John Bocco ambaye alikosa.

Kutokana na vurugu hizo mchezaji wa Ruvu Shooting, Shaaban Msala alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati ila BM hakuonyeshwa kwa kadi kwa kile ambacho ilionekana mwamuzi hajaona tukio hilo lililorushwa moja kwa moja na Azam Tv.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here