Mlipuko wauwa wanajeshi watatu wa Ufaransa Mali

0

WANAJESHI watatu wa Ufaransa wameuwa, baada ya gari walilokuwemo kushambuliwa kwa bomu jana, huko katika mkoa wa Hombori uliyopo katika eneo la katikati ya Mali.

 Idadi hiyo ya vifo inafanya jumla ya vifo ya wanajeshi wa Ufaransa waliuwawa nchini Mali tangu tangu waingie kwa mara ya kwanza Januari 2013 kufikia 47.

 Taarifa ya ofisi ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron imesema imetoa heshima kubwa ya kuwakumbuka wanajeshi hao. Na kwamba kilichotokea kinaongeza nguvu zaidi ya kukabiliana na ugaidi.

Kikosi cha Ufaransa cha Barkane katika eneo la Sahel kina jumla ya wanajeshi 5,100 na kimekuwa kikipigana bega kwa bega na wanajeshi wa mataifa ya Mauritania, Chad, Mali, Burkina Faso and Niger, ambayo yanaunda kundi la mataifa ya G5 ya eneo hilo la Sahel.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here