Mkuu wa WHO aonya dhidi ya ‘utaifa wa chanjo’

0

NEWYORK, MAREKANI

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito wa mshikamano wa kimataifa katika uzinduzi wa chanjo yoyote ya virusi vya corona katika siku za usoni, wakati idadi ya maambukizi ikiongezeka kote duniani.

Katika hotuba ya video wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Afya Duniani mjini Berlin hapo jana, Ghebreyesus alisema njia pekee ya kujikwamua kutokana na janga hilo ni kushirikiana na kuhakikisha kuwa nchi maskini zina fursa sawa ya kupata chanjo.

Wanasayansi kote duniani wanapambana kutengeneza chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, ambao umewauwa zaidi ya watu milioni 1.1.

Umoja wa Ulaya, Marekani, Uingereza, Japan na mataifa mengine kadhaa tayari yameweka oda kubwa na makampuni yanayohusika na utengenezaji wa chanjo zinazoonekana kuwa bora.

WHO imeripoti jana siku ya tatu mfululizo yenye maambukizi mengi kote duniani, na kuzitaka nchi kuchukua hatua zaidi ya kusambaa kwa ugonjwa huo. Zaidi ya visa 465,319 vimetangazwa Jumamosi pekee, nusu ya idadi hiyo ikiwa barani Ulaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here