Mkuu wa WHO ajiweka karantini

0

GENEVA,USWISI

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema anajiweka karantini baada ya kukutana na mtu ambaye sasa amebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Tedros ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kwamba yuko kwenye afya njema bila dalili za maambukizi ya virusi vya corona, lakini atakaa kwenye karantini kwa siku kadhaa zijazo kama taratibu za WHO zinavyoelekeza.

Mkuu huyo wa Shirika la Afya Duniani, amesema ni muhimu kuzingatia miongozo ya wataalamu wa afya kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Wiki iliyopita aliwatolea wito viongozi wa dunia kuzingatia ushauri wa wataalamu katika wakati ambapo idadi ya maambukizi inapanda barani Ulaya na kwenye mataifa ya Amerika Kaskazini.

Ofisi za WHO zipo mjini Geneva ambako takriban watu 1,000 wameripotiwa kuambukizwa kwa siku katika mji huo wenye wakazi wapatao laki tano

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here