Mkutano Baraza la wawakilishi kuanza leo

0
Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi jumatano anatarajia kulihutubia na kulifungua rasmi Baraza la 10 la Wawakilishi ambapo leo mkutano wa kwanza wa Baraza la 10 la Wawakilishi linatarajia kuanza visiwani hapa.

Kuanza kwa shughuli za mkutano wa Baraza hilo la 10 la Wawakilishi Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Raya Issa Msellem alisema katika mkutano huo ambao unatarajia kuanza leo utafuatiwa na shughuli ya uchaguzi wa Spika wa Baraza la Wawakilishi.

Katibu huyo alisema shughuli za mkutano wa baraza hilo la 10 linatarajia kuanza saa nane mchana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Chukwani mjini Unguja ambapo pia kunatarajiwa kuwepo kwa uchaguzi wa Naibu Spika.

“Katika shughuli za mkutano huo zitakuwa kama zifuatavyo itatangulia na tangazo la Rais wa Zanzibar kuitisha Baraza la 10 la Wawakilishi,Spika kuapa kiapo cha uaminifu,kiapo cha uaminifu kwa Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi na mwishoni ni shughuli nyingine itakayojitokeza,”alisema

Akiwataja wagombea wa nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi ambao hadi sasa wameshachukua fomu na kurejesha ni Zubeir Ali Maulid wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Ali Makame Issa kutoka CUF,Naima Salum Hamad wa chama cha UDP,Ameir Hassan Ameir wa Demokrasia Makini pamoja na Hamad Mohamed Ibrahim wa chama cha UPDP.

Katibu huyo alisema tayari Baraza la Wawakilishi limeshapokea taarifa ya wajumbe wateule wa Baraza hilo la Wawakilishi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) katika chama cha CCM na ACT-Wazalendo na kwamba mpaka sasa vyama hivyo vimeshapokea taarifa hizo na hakuna chama ambacho kimewasilisha taarifa ya kukataa.

“Mpaka sasa idadi ya viti maalum ni 18 ambavyo viti hivyo vyote vimetokea CCM na kwa wawakilishi wa majimbo CCM ina viti 46 na CUF kiti kimoja na ACT-Wazalendo viti tatu,”alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here