Mkurugenzi Kigoma amuumbua Zitto

0

NA MAGRETH MAGOSSO, KIGOMA

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Kigoma Ujiji Mwailwa Pangani amemtaka Mgombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe,asiweweseke na kuipaka matope Tume ya uchaguzi ya Taifa kwa kusambaza taarifa za ulongo kwa wananchi kupitia mitandao ya kijamii.

Akitoa kauli hiyo ofisini kwake kigoma ujiji,mbele ya wandishi wa habari kwa lengo la kukanusha taarifa hizo zenye propaganda za kuichafua tume ya uchaguzi kwa kuwa alikuwa na nafasi ya miezi sita  hapo nyuma ya kuweka pingamizi dhidi ya tuhuma  zake.

“Zitto haitakii mema Halmashauri yetu.wapiga kura hewa  elfu 13,330 katika daftari la kupiga kura.taarifa hizi si za kweli wapiga kura wote wapo kwenye  daftari la mpiga kura hao wanafunzi na askari wa kujenga taifa, ni ulongo wenye nia ovu ya kuipaka matope tume ya uchaguzi Taifa.”alisema.

Alieleza kuwa katika Manispaa ya kigoma ujiji kuna wapiga kura waliokidhi vigezo ambao wapo kwenye daftari la kupiga kura ni Laki 128,365 na kuna Shule  za tatu tu,za kidato cha sita ambazo ni Buronge,Kichangachui na kigoma na wenye sifa za kupiga kura hawazidi  elfu 2,000 huku alisisitiza wananchi wapuuze taarifa hizo.

Alimtaka Mgombea huyo aache siasa za uchonganishi dhidi ya wananchi na serikali yao na kumshauri afanye siasa zenye mashiko kwa jamii ya kigoma mjini,badala ya kueneza propaganda za uongo kwa kutumia umaarufu wake wa kushawishi uovu .

Aidha alisema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa tamko kwa wakurugenzi watakaoharibu matokeo ya uchaguzi watagharamia zoezi hilo upya kwa gharama zao wenyewe.sababu uchaguzi unagharamiwa na fedha za ndani.kwa hali hiyo afanye kampeni kwa kunadi sera na si vinginevyo.

Alisema ,vyama 15 vinashiriki uchaguzi na Octoba 26, Mwaka huu watafanya ziara ya pamoja na wanasiasa husika katika kukagua vituo vya uchaguzi.

Alifafanua kuwa,ametumia vyombo vya habari kwa kuwatoa hofu wananchi huku akitarajia kuketi na kamati ya chama kulizungumzia hilo na asitafute sababu zisizo na mashiko kwa umma na kumtaka  aendelee kufanya siasa zake bila kukiuka sheria,taratibu na kanuni husika.

Ikumbukwe,Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter juzi aliwaacha watu na sintofahamu ya kile alichodai, “Katika Jimbo langu kuna wapiga kura 13,830 wameongezwa kwenye daftari la wapiga kura. Kura zao zitapigwa na askari wa JKT na wanafunzi walioandaliwa. Nataka kumwambia Mkuu wa Usalama wa Taifa Athumani kuwa,kigoma mjini atakachokipata”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here