Mkurugenzi Igunga uteuzi wake watenguliwa

0

Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Bw. Revocatus Kuuli.

Utenguzi huo umefanyika leo Jumatatu Disemba 28, 2020 wakati Rais Magufuli aliposimama kuwasalimu wananchi wa Igunga wakati akiwa safarini ambapo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Phillemon Sengati kuteua mtumishi mwadilifu atakayekaimu nafasi hiyo mpaka hapo uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji utakapofanyika.

Rais   Magufuli   amesema   pamoja   na   malalamiko   mengi kutoka kwa wananchi, anazo taarifa nyingi za dosari za Kuuli na kwamba alishamuonya juu ya vitendo vyake vya kuwadhulumu wananchi wakiwemo wanawake na kueleza Serikali anayoiongoza haiwezi kumvumilia kiongozi wa namna hiyo.

Kuuli anakabiliwa pia na tuhuma za utendaji kazi usioridhisha na ubadhirifu wa fedha za maduhuli ya Serikali.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here