Mitihani ya taifa yaahirishwa Nigeria kutokana na ghasia

0

Lagos, NIGERIA 

Baraza la Mitihani nchini Nigeria (NECO), imehairisha mtihani wa taifa kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho huku ghasia zikiendelea kati ya waaandamanaji wanaopinga unyama unaotekelezwa na polisi na maafisa wa usalama nchini humo.

Barazal hilo limesema uamuzi wa kuahirisha mitihani pia umetokana na hatua ya baadhi ya majimbo kuweka amri ya kutotoka nje.

Mji wa Lagos na sehemu zingine nchini humo zimeshuhudia majengo yakichomwa moto, maeneo ya kibiashara yakiporwa na magereza yakivamiwa tangu waandamanaji walipopigwa risasi Jumanne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here