Home HABARI Mitaa, mabasi jijini Dar kupuliziwa dawa ya kuua vimelea vya corona

Mitaa, mabasi jijini Dar kupuliziwa dawa ya kuua vimelea vya corona

NA MWANDISHI WETU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kupuliza dawa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, ili kuua vimelea vya magonjwa ikiwemo Virusi vya ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 24, 2020 alipotembelea kituo kikuu cha mabasi Ubungo na kukagua kama watoa huduma wa usafiri huo wameweka vitakasa mikono (hand sanitiser) ili kujikinga na ugonjwa wa corona Makonda amesema mkoa huo utaanza kupuliza dawa hiyo kuanzia kesho Machi 25.

“Dar es Salaam, tunaanza kupuliza dawa wiki hii kwenye maeneo mbalimbali ya jiji ili kuua vimelea vya magonjwa ikiwemo Virusi vya Corona, nawaomba wananchi watoe taarifa mapema endepo wataona mtu mwenye dalili zinazofanana na zile na ugonjwa wa Corona,” amesema Makonda.

Aidha Makonda amewataka abiria wanaotumia kituo hicho kuchukua tahadhari ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

“Mabasi yote hapa Ubungo ni lazima yawe na vitakasa mikono na yapuliziwe dawa kabla ya kuanza safari na kumaliza safari na elimu itolewe kuhusu Virusi vya Corona na mabasi yote mtapata ‘clip’ za video ambazo zinatoa elimu kuhusu ugonjwa huu.”

Makonda pia ameongeza; “unapolazimisha kupanda daladala iliyojaa humkomoi mtu unahatarisha maisha yako mwenyewe, inawezekana unaenda kununua mauti kwa kusimama kama abiria kwenye daladala.

“Kwa kipindi hiki niwaombe tuvumilie acha daladala iliyojaa iondoke, subiri ambayo haijajaa, ni bora kuchelewa utafika kuliko kujidai unawai ukaleta madhara ya maisha yako.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments