Miss Tanzania 2020 ni Rose Manfere

0

Rose Manfere mwenye umri wa miaka  21 ametangazwa kutwaa taji la Miss Tanzania usiku wa kuamkia leo Jumapili Desemba 06, 2020.

miss tz picNafasi ya pili imenyakuliwa na mrembo Juliana Rwehimiza na nafasi ya tatu akiibeba  Prisca lyimo.

Kutokana na ushindi huo, Rose amezawadiwa gari aina ya Toyota Subaru Impreza toleo la Mwaka 2011 lenye thamani ya Sh13 milioni.

Wakati mshindi wa pili Juliana ataondoka na seti ya sofa na meza ndogo ya sebuleni.

Mashindano hayo yaliyoanza Saa 4:00 usiku, yalihitimishwa Saa 8 usiku na mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here