Mikel Arteta : Wiki ijayo ni muhimu kwa Arsenal

0

ENGLAND, UK

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amesema wiki ijayo itakuwa muhimu kuhakikisha timu yake haijipati katika hali ya kushukishwa daraja.

Gunners wamefanikiwa kushinda mechi moja katika michezo 10 ya Ligi ya Premia, ambayo imeifanya kushuka hasi nafasi ya 15 katika msimamo wa jedwali la EPL.

“Sitaki kutoa udhuru wowote,” alisema Arteta, ambaye alimrithi Unai Emery alipofutwa mwezi Decemba 2019.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 38- anaungwa mkono na uongozi wa Arsenal.

Gunners waliwakaribisha Chelsea jana Jumamosi na kisha watakutana na – Brighton, ambao ushindi wao pekee nyumbani mwaka 2020 ulikuwa dhidi ya Arsenal msimu uliopita, na West Brom.

Alipoulizwa kama wiki ijayo ni muhimu ikiwa timu yake haitaki kushuka daraja, Arteta alisema: “Ndio, kabisa. Siku saba hadi nane zijazo zitakuwa muhimu kuona ni wapi tutaelekea katika Ligi Kuu. “

Baada ya kumaliza msimu uliyopita kwa kushinda kombe la FA , kisha kuanza msimu huu kwa kunyakua taji la Community Shield, kushinda mechi tatu kati ya nne za ufunguzi wa ligi na kuinyuka Leicester na Liverpool katika kombe la Carabao, mchezo wa Arsenal umedorora vibaya.

Mkufunzi wa West Brom Sam Allardyce siku ya Jumatano alisema anaichukulia Gunners kama mpinzani kutoka chini.

Arteta anasema: “Nimekuwa wazi mara nyingi kwanini tunashindwa mechi zetu. Ni jukumu langu kuweka hilo wazi, bila kujali ni nini kitatokea, ni sisi tumejishusha na ni jukumu letu kubadilisha hilo.”

Wapinzani wa Jumamosi Chelsea walijibu kupoteza fainali ya Kombe la FA msimu uliopita dhidi ya Arsenal kwa kutumia pauni milioni 200 kuwasajili wachezaji wapya.

Asernal inafanya vibaya katika msimu huu tangu kuondoka kwa kocha wa muda mrefu Aserne Wenger ambapo katika msimamo wa ligi inashika nafasi ya 15 ikiacha nafasi mbili tu kushuka daraja. Imecheza jumla ya mechi 14 ikiwa na alama 14 baada ya kushinda mechi nne, kutoka sare mbili na kufungwa mechi nane.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here