Miamba ya soka kuwania tuzo za ubora karne ya 21

0

LONDON, UINGEREZA

MIAMBA ya Soka Duniani, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Ronaldinho Gaucho na Mohamed Salah wanawania tuzo ya mchezaji bora wa karne ya 21 kwenye Tuzo za Soka za ulimwengu (Dubai Globe Soccer Awards), baada ya kupigiwa kura milioni nane ulimwenguni kote kutoka nchi zaidi ya 230.

Cristiano, Messi na Lewandowski pia wameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa 2020.

Pamoja na tuzo za mtu binafsi, kutakuwa pia na tuzo kwa klabu bora ya karne ya 21, ambapo Miamba ya Misri Al Ahly wataminyana na Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid kuwania tuzo hiyo ya klabu bora ya karne ya 21.

Tuzo hizi zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu mwaka 2010, ambapo tuzo hii imekuwa ikitolewa kwa kocha bora, timu bora wakala bora. Tuzoa za mwaka huu zitatangazwa Disemba 27, 2020 na ni kwa mara ya kwanza washindi watapatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki.

Hii hapa orodha ya Tuzo zinazowaniwa kwa upande wa tuzo za ubora kwa Karne ya 21.

Tuzo mchezaji bora wa Karne wanao wania: Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Ronaldinho na Mohamed Salah.

Tuzo kocha bora wa Karne wanao wania ni: Sir Alex Ferguson, Pep Guardiola, Jose Mourinho na Zinedine Zidane.

Tuzo klabu bora ya Karne timu zinazowania ni: Al Ahly, Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid.

Tuzo ya wakala bora wa Karne wanao wania ni: Giovanni Branchini, Jorge Mendes na Mino Raiola

Tuzo nyingine zitakazo tolewa hiyo Disemba 07, 2020 ni tuzo za ubora kwa mwaka 2020.

Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora 2020 wanaowania ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Robert Lewandowski.

Tuzo klabu bora 2020 timu zinazowania ni Bayern, Liverpool and Real Madrid.

Tuzo kocha bora 2020 wanaowania ni Gian Piero Gasperini (Atalanta), Hansi Flick (Bayern) na Jurgen Klopp (Liverpool).

Mwaka 2019, tuzo ya kocha bora ilienda kwa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, Cristiano Ronaldo alishinda tuzo ya mchezaji bora na Jorge Mendes alishinda tuzo ya wakala bara wa nwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here