Miaka 59 ya Uhuru: Magufuli abeba ajenda za uhuru

0

Kipindi cha Ukoloni, waasisi wetu waliamua kutafuta Uhuru kwa dhumuni la kujitawala, kujitegemea na kujiletea maendeleo

Na Mwandishi Maalum

LEO Tanzania imefikisha miaka 59 ya Uhuru, ambao ulitokana na kufanikiwa kuwaondoa Waingereza, ambapo Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwaambia Watanganyika(Watanzania) enzi hizo kuwa lazima wadai Uhuru ili waweze kujikomboa.

Dira na malengo ya Hayati Mwalimu Nyerere ilikuwa ni kujikomboa na kuondokana na umaskini uliokuwepo enzi hizo, hivyo Desemba 9, 1961 ilikuwa ni safari ya matumaini kwa watanzania kuwaondoa wakoloni ili kujitawala, kujitegemea na kujiletea maendeleo.

Miaka 59 ni miaka mikubwa na yenye maendeleo makubwa kwa wananchi, ambao waliokuwepo 1961 wamekuwa na ushuhuda mkubwa wa namna Rais Dk. John Magufuli alipoweza kubebea agenda za maendeleo za watanzania, ambazo Hayati Mwalimu Nyerere alizijenga na kutaka kuzifikia.

Mengi yamefanyika katika kipindi cha miaka 59, toka awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, ikajaa awamu ya pili ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu ya Rais Mstaafu, Hayati Benjamini Mkapa, awamu ya nne ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Marais hao wote wamefanya makubwa kwa watanzania katika kutimiza agenda na malengo ya Uhuru kwa Tanzania, ambapo awamu ya tano chini ya Rais Dk. Magufuli imeweza kuifikia malengo hayo kwa kuweza kuishi kwenye matamani na mahitaji ya awamu zote za tawala za Tanzania.

Rais Dk. Magufuli ameweza kufikisha Tanzania katika kilele cha mafanikio hasa kwenye kipindi cha miaka 59, ambapo ndani ya miaka mitano yake ya utawala ameweza kukamilisha dira ya malengo ya maendeleo ya taifa kuafikia uchumi wa kati kabla ya 2025.

Miaka 59 ya Uhuru na 58 ya Jamhuri ni kipindi kirefu ambacho mabadiliko makubwa yameonekana yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa ujumla, ambapo Wakati Tanganyika inapata mwaka 1961 hadi hivi sasa Tanzania imekuwa bora kwenye kila sekta.

Ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mikubwa ikiwemo ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Julius Nyerere ulioko Rufiji, mkoani Pwani, Ujenzi wa Reli ya kisasa yenye viwango vya kimataifa (SGR) na miradi mikubwa ya barabara, madaraja, hospitali na majengo kwenye kila maeneo tumeweza kuifikia agenda za Uhuru.

Wakati Tanganyika inapata uhuru, kuliuwepo na matatizo lukuki kwenye kila sekta, lakini sas a mafanikio makubwa yamepatikana chini usimamizi madhubuti wa Rais Dk. Magufuli, ambapo amekuwa kiongozi mwenye maono makubwa ya kuleta uchumi wa Tanzania na hata nchi kusimama imara kwenye miaka 59 ya Uhuru.

Ikumbukwe kuwa ili Taifa liweze kuendelea vipo vitu muhimu takriban vinne, Siasa Safi na Uongozi bora, Ardhi na watu. Watu ndio nguvukazi, ndio soko la bidhaa, hivyo nchi yenye idadi kubwa ya watu, pamoja vitu vingine ina uhakika wa nguvu kazi na soko la uhakika la ndani.

Tanganyika ilipopata uhuru kulikuwepo takriban watu milioni 9 na miaka 59 baada ya uhuru, nchi hii ina zaidi ya watu milioni 55, ambapo matumizi bora ya nguvu kazi hiyo imekuwa ni jibu mujaraba katika maendeleo ya Watanzania ambao wamekuwa bora na wenye kusherehekea mafanikio hayo.

Maendeleo hayo yamejidhihirisha kila sehemu, ambapo Rais Dk. Magufuli ameweza kuyafikia ikiwemo utoaji wa elimu bura, usambazaji wa umeme vijijini huku kukiwa na mafanikio makubwa kwenye kila nyanja ikiwemo kutoka kilometa 360 za lami enzi za Uhuru hadi kilometa 14,000 za lami hivi sasa.

Zaidi ya hayo Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na makimbilio ya nchi jirani ambazo zimekuwa zikikumbwa na machafuko ya kisiasa na kikabila. Amani hii lazima ilindwe kwani ni mtaji wa maendeleo na ndio maana Rais Dk. John Magufuli amekuwa akisisitiza muda wote kuwa amani ya nchi kulindwa zaidi.

Miaka 59 ya Uhuru na 58 ya Jamhuri imetumika kwa watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujitegemea kiuchumi sawa na Kaulimbiu ya maadhimisho ya Uhuru mwaka huu isemayo “MIAKA 59 MIAKA 58 YA JAMHURI TANZANIA YENYE UCHUMI IMARA ITAJENGWA NA WATANZANIA WENYEWE, TUFANYE KAZI KWA BIDII, UWAJIBIKAJI NA UADILIFU”.

Ujinga, maradhi na Umaskini, Mwalimu Nyerere alisisitiza juu ya mambo haya makuu matatu, kama sehemu kubwa ya kupambana na kuiondosha Tanzania, ambayo Rais Dk. Magufuli ameweza kuiondosha na kuwa mfano mmoja wapo wa kuleta maendeleo kwa taifa.

”nchi hii ni bado ya wakulima na wafanyakazi, hatuwezi kuwa nchi ya watu wenye kudai na kudai, nawaomba ndugu zangu watanzania hatujalemaa sana, lakini kilema kipo, viongozi wetu wanadai na kudai tuu, watu ni maskini, wachache hao wana nguvu ya kuongoza nchi hii ndio wanaodai tuu” alisema Hayati Nyerere.

”Katika miaka 59 ya Uhuru na katika miaka mitano ya uongozi wa Rais Magufuli kama kuna eneo tumewekeza kwa kiasi kikubwa na limesaidia sana kuchemsha uchumi ni katika ujenzi ambao wengine wanaita maendeleo ya vitu. Kwa mfano unapozungumzia mradi wa umeme wa Rufiji umebuni ajira ya zaidi ya 3500”, alisema Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abass ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here