Miaka 20 jela kumuingizia mtoto vidole sehemu za siri

0

Na DEVOTHA FULUGUNGE

MKAZI wa Mbezi juu, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Dotto Bakari  amehukumiwa kifungo cha miaka (20) jela baada ya kukutwa na hatia ya ubakaji hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Hudi Hudi.

Hakimu Hudi alimtia hatiani Bakari (49) na kumpatia adhabu ya kwenda  jela miaka 20 pamoja na adhabu kali .

Mshitakiwa huyo alihukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 18.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa alidai wa kutenda kosa hilo  septemba 15 mwaka 2018 ,huko maeneo ya Mbezi juu Beach Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam kuwa aliingiza vidole vyake sehemu ya uke wa mtoto mwenye  umri wa miaka 4 .

Kwa upande wa Jamhuri, wakili wa serikali Daisy Makakala aliiomba Mahakama kumpatia adhabu kali mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na jamii kwa ujumla.

Hakimu Hudi alimruhusu mshtakiwa kujitetea mbele ya Mahakama kwa ajili ya  kupunguziwa adhabu na Mahakama hiyo.

Mshtakiwa aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kutokana na ugonjwa alionao mbali na hapo alidai kuwa yeye ni baba wa familia.

Hakimu Hudi alisema “kutokana na Mahakama kumtia hatiani mshtakiwa Mahakama inakupa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela  na adhabu kali”.

Wakati huo huo washitakiwa Rajabu Boi(30), Beatus Alex(25), Japhet Kabuge(30) na Andrew Munde (25) wote wakiwa ni wakazi wa Bunju “A”katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 mbele ya Hakimu Mkazi Hudi Hudi na wakili wa serikali Daisy Makakala kwa shitaka la unyang’anyi kwa kutumia silaha .

Washtakiwa hao wote kwa pamoja wametiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha  kwa ushahidi wa upelelezi toka pande zote.

Shtaka linalowakabili washitakiwa hao ni kuwa Januari10 mwaka 2019 ,eneo la Bunju “A” katika Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam kuwa waliiba simu aina ya Samsung Galaxy j6 pro yenye thamani ya sh.700,000, simu aina ya Samsung Galaxy j7 yenye thamani ya sh 850,000, runinga mpanguso aina ya Samsung yenye thamani ya sh 760,000 na pesa taslimu kiasi cha sh. 450,000 na vyote vikiwa na thamani ya sh 2,760,000 mali ya F.4824D/CPL. Joseph na kabla na baada ya kufanya wizi huo walimtishia kwa panga ili waweze kujimilikisha mali hizo.

Kabla ya Hakimu Hudi kutoa hukumu hiyo  aliwapatia washtakiwa nafasi ya kujitetea mbele ya Mahakama ili wapunguziwe adhabu na Mahakama hiyo.

Mbali na hapo, washtakiwa hao hawakuwa na utetezi utetezi wowote  juu ya hukumu yao hivyo wakili wa serikali Daisy Makakala aliiomba Mahakama kuwapa adhabu kali ili iwe fundisho katika jamii.

Hakimu Hudi aliwahukumu washtakiwa hao kifungo cha miaka 30 jela sambamba na adhabu kali

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here