Mgogoro wa Ethiopia wavuka mpaka huku maelfu wakikimbilia Sudan

0

NAIROBI, Kenya

MZOZO wa Serikali ya Ethiopia na jimbo lake la Kaskazini la Tigray umevuka mpaka juzi baada ya maelfu ya watu kuhamia nchini Sudan, pamoja na wanajeshi wanaotafuta ulinzi. Karibu wakimbizi 3,500, wakiwemo wanawake na watoto wamewasili katika mkoa wa Kassala nchini Sudan, na wengine wako njiani.

Kufikia juzi jioni, idadi ya Waethiopia wanaokimbilia mkoa huo wa mpakani ilipindukia 6,000 kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan – SUNA. Zaidi ya Waethiopia 200,000 wanatarajiwa kuvuka mpaka na kuingia Sudan katika siku chache zijazo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekataa miito ya jamii ya kimataifa ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Tigray, akisema hakutakuwa na mazungumzo hadi pale operesheni ya utekelezaji wa sheria itakapokamilika.

Analenga kuwakamata wakuu wa serikali ya kikanda ambayo utawala wake unaichukuliwa kuwa kinyume cha sheria wakati pia akiziharibu zana zake za kivita. Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa katika pande zote za mgogoro huo mpaka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here