Mesut Ozil: Je hii ndio sababu ya kiungo huyo kuwachwa nje ya kikosi cha Arsenal?

0

LONDON, UINGEREZA

KIUNGO huyo wa kati alyewahi kushinda kombe la dunia Mesut Ozil amewachwa nje ya kikosi cha ligi ya Premia na kile cha kombe la Yuropa na kusema kwamba utiifu ni vigumu kuupata siku hizi.

Mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta alisema kwamba amefeli kuelewana na kiungo huyo mchezeshaji wa Ujerumani na kwamba kuwachwa kwake nje ni uamuzi wa timu.

Hatahivyo baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamesema kwamba kuwachwa kwake nje kunatokana na matamshi yake kuhusu mateso wanayopitia Waislamu wa kabila la Uighurs nchini China.

Katika taarifa yake katika mtandao wa kijamii siku ya Jumatano , Ozil mwenye umri wa miaka 32 aliandika:

”Nitaendelea kuifanya mazoezi na kutumia sauti yangu dhidi ya ukiukaji wa haki za kibinadamu ili kutetea haki”.

Je ni nini kilichosababisha matamshi hayo ya China?

kilichotokea

Mwaka 2018, uchunguzi wa BBC ulibaini kwamba takriban watu milioni moja wengi wao kutoka katika jamii ya Uighurs walio Waislamu nchini China walidaiwa kukamatwa na kuzuiwa bila kushtakiwa katika jela kubwa.

Disemba iliopita Ozil, ambaye ni Muislamu , alitoa chapisho katika mtandao wa kijamii akiwaita watu wa jamii ya Uighurs mashujaa ambao wanakataa kushtakiwa huku akiikosoa China na Waislamu walionyamaza.

Arsenal ilijiondoa kutokana na matamshi ya Ozil ikisema klabu hiyo haingilii masuala ya kisiasa.

China mara kwa mara imekataa kuwatesa watu wa jamii ya Uighurs nchini humo `na kusema kwamba wanasomeshwa katika vyuo tofauti ili kukabiliana na misimamo mikali ya kidini miongoni mwao.

Baada ya chapisho hilo , Ozil aliondolewa katika video ya pro Evolution soccer 2020 na mechi ya Arsenal dhidi ya Man City ikaondolewa katika matangazo ya moja kwa moja ya chombo cha habari cha CCTV.

Msemaji wa waziri wa masuala ya kigeni nchini China alisema kwamba Ozil amedanganywa na habari bandia hatua iliomfanya kutoa matamshi hayo.

Je ameichezea Arsenal tangu matamshi hayo ya kwanza?

Mesut Ozil

Ozil alichapisha picha hii katika mtandao wa kijamii wiki iliopita.

Ozil alikuwa amewachwa nje na mkufunzi aliyeondoka Unai Emery kabla ya kurudi katika ,kikosi hicho chini ya ukufunzi wa kaimu meneja Freddie Ljungberg mwanzo wa mwezi Disemba 2019.

Baada ya kuajiriwa kwa Arteta kuwa mkufunzi wa kudumu baadaye mwezo huo , mwezi ambao Ozil alitoa matamshi hayo, mchezaji huyo wa Ujerumani alianzishwa katika mechi 10 za ligi ya Premia kabla ya mlipuko wa corona kusababisha likizo ya miezi mitatu mnamo mwezi Machi , lakini hajaonekana akivalia tishati ya Arsenal.

Tangu alipojiunga na Arsenal kutoka Real Madrid miaka saba iliopita , Ozil amefunga magoli 44 katika mechi 254 katika madhindano yote akiichezea Arsenal.

Alisema siku ya Jumatano kwamba amekasirishwa na hatua ya kutoshirikishwa katika mechi za Premia katika msimu huu.

”Baada ya kuandikisha kandarasi mpya 2018, niliahidi kutii klabu hii, naipenda Arsenal na inanihuzunisha kwamba hilo halifikiriwi,”.

Arteta ajibu tuhuma za Mesut Ozil

Hatimae meneja wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta, anamjibu kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil, kufuatia waraka aliousambaza kwenye mitandao ya kijamii mapema juma hili.

Ozil alisambaza waraka wa kuachwa kwake katika mtandao wa kijamii baada ya kuvuja kwa taarifa kuwa Arsenal imemuengua kwenye orodha ya wachezaji watakaiwakilisha klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu.

Arteta amesema Ozil ameshindwa kumuheshimu kwa tukio hilo, huku akimtaka ajilaumu mwenyewe kwani hajatimiza majukumu yake kama mchezaji.

Meneja huyo ambaye aliwahi kutumikia Arsenal kuanzia mwaka 2011 hadi 2016 amesema, Ozil ameleta vita ndani ya klabu ambayo haina ukweli, kwa kulituhumu benchi la ufundi kwa kukosa heshima na kuona thamani yake.

Arteta amesisitiza kuwa, Ozil hana mtu wa kumlaumu zaidi ya yeye mwenyewe, akimaanisha kuwa kiungo huyo kutoka amemalizana rasmi na klabu hiyo.

“Kitu kinachotokea kwa Ozil kwa sasa si kitu kipya. Hali niliyomkuta nayo wakati najiunga na klabu hii ilikuwa ngumu, mambo haya yamekuwa yakitokea kwa miaka minane sasa.”

“Kazi yangu ni kuimarisha viwango vya wachezaji kuleta timu bora uwanjani, lakini kwa sasa nahisi kama nimefeli. Nilimuhitaji Ozil mwenye kiwango bora na wakati tukimaliza mchakato, sikuwa na uwezo wa kumaliza hilo kwa ubora kwa sababu nilitakiwa kufanya uamuzi na kumwacha nje ya kikosi.”

 “Hilo halihusiani na tabia ya mtu wala suala la mshahara kama ambavyo nimekuwa nikisoma katika mitandao. Hilo halina ukweli wowote.”

“Nimeajiriwa kama kocha kwa ajili ya kushinda mechi za klabu hii na natakiwa kufanya uamuzi kupata timu bora kutoka katika timu hii.” Amesema Arteta.

Arteta usiku wa kuamkia leo alikiongoza kikosi cha Arsenal kushinda mchezo waked wa kwanza wa UEFA Europa League kwa kuichabanga Rapid Wien mabao mawili kwa moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here