Meli kutoka DRC yawasili Kigoma

0

Na Magreth Magosso, Kigoma 

WASAFIRISHAJI wa bidhaa mbalimbali kutoka Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Zambia na Burundi wameondokana na kadhia ya ucheleweshwaji wa usafirishwaji wa bidhaa zao kupitia Bandari ya kigoma, baada ya ujio wa Meli kubwa (Mv-Amani) wa ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki kutua kigoma tayari kwa usafirishaji wa bidhaa mtambukwa.

Wakizungumzia hilo kwa nyakati tofauti baadhi ya wasafirishaji wa mizigo kutoka kigoma kwenda Drc Kongo waishio Manispaa ya kigoma Ujiji hawakusita kuzipongeza  serikali mbili ya Tanzania na Kongo katika kuchagiza uchumi wa wananchi wao.
Bushiri Juma ni mfanyabiashara na msafirishaji wa bidhaa ya Chumvi kutoka kigoma kuelekea Kongo kwa miaka 30 alisema,awali waliathirika kiuchumi na kushindwa kuondokana na tope la ufakiri kutokana  na ucheleweshwaji na sintofahamu wa muda wa  mizigo yao kufika eneo husika kwa wakati.
“Mzigo unakaa bandarini zaidi ya miezi miwili hadi mitatu.unalowa na mvua kipindi cha masika.unakosa fedha ya kulipia nyumba ya kulala wageni wakati unasubiri usafiri hali iliyotunyima fursa ya biashara kuwa na wigo mpana.alisema.
Juma Chaulembo ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Kigoma alidhihirisha furaha yake kwa serikali hizo na kueleza kuwa,sura mpya ya uchumi kuchagizwa na Mv Amani yenye uwezo mkubwa wa kubeba shehena kubwa ya mzigo na abiria.
“Serikali ya Congo imefungua fursa ya biashara  na tunamini biashara itaongezeka kwa kasi na ufanisi  wa muda utakuwa rafiki na uhakika wa biashara kuchagiza Maendeleo ya wananchi nufaika”alisema.
Sendwe Mbarouk ni Mwenyekiti wa usafirishaji wa Mizigo kwa Maboti ya asili Kigoma.alipohojiwa juu ya ujio wa Meli hiyo alisema,changamoto ya hali ya hewa iliyokuwa ikiharibu bidhaa za wateja wao itapungua kwa kiasi  kikubwa mno.
“Ziwa tanganyika kwa upande wa kusini wafanyabiashara na sisi wenye Maboti tuliathiriwa na hali ya hewa.ambapo upepo ukivuma sana ilibidi tutupe baadhi ya mzigo ili kujinusuru na kuzama kwa boti unafahamu ajali zinazojitokeza za boti za mizigo na abiria nyingi ni Kigoma kuzini.”alisema.
Alifafanua kuwa, ili Mv-Amani  iwasaidie na watu wa kigoma kusini.serikali haina budi kuboresha miundombinu  ya vivuko vya bandari  hasa kusini ambao wasafiri na asafirishaji wanatumia usafiri wa boti za asili na iwekeze kwa vyama vya wadau wa usafiri huo ili  uongeza tija ya usafiri wa majini kwa kuwa ziwa tanganyika ni chachu  katika  uchumi wa wananchi wa serikali zote mbili.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mv Amani ya DRC Congo Solomon Masuma alisema sababu kubwa ya kuwekeza Kigoma ni jitihada ya kumuunga mkono na kutimiza ndoto ya Rais John Magufuli juu ya usafiri wa uhakika na salama ziwa tangantika si Siasa kama wengi wanavyodhani.alitaka Kigoma uwe Mji wa Biashara.kabla ya miaka mitano.
“Rais Magufuli alitaka atimize hilo kupitia wadau sekta binafsi ina mchango mkubwa wa kuisaidia serikali kukamilisha mipango yake, meli hii inabeba tani 3,500 ya mzigo, gari zaidi ya 50,vyumba vya kulala zaidi ya 22 ndani ya masaa manne hadi matano upo kigoma aidha Kalemie.”alisema.
Aidha, anafungua fursa ya biashara kwa wafanyabiashara wa Tanzania wa mazao ya mifugo, kilimo lakini kuna nafasi ya ajira kwa kuwa kuna kitengo cha mgahawa, wauguzi ambayo ni fursa kwa pande mbili ya serikali hizo.kwa kuwa wana tawi lao hapo.alibainisha.
Akiongezea hilo Meneja wa Bandari Kigoma,akiri meli hiyo ni suruhisho la ucheleweshwaji wa bidhaa zao kwa kuwa inahudumia Shehena kubwa na kwa wakati ile kadhia ya mizigo kukaa muda mrefu na kuongeza gharama za usafirishaji inatoweka.
Akipokea Meli hiyo mwishoni mwa wiki,katika viwanja vya bandari ya kigoma, Mkuu wa Mkoa, Thobias Andengenye alisema, usafiri rahisi wenye gharama nafuu ni usafiri wa maji.
Hivyo, alitoa rai kwa wananchi wachangamkie fursa waibue maendeleo ya kiuchumi.serikali ikiendelea kuimarisha miundombinu ya usafishaji hadi sasa kiasi cha fedha Bilioni 10 kimetengwa kwa ajili ya meli mpya ya abiria na mizigi.kuikarabati meli kongwe ya MV Liemba sambamba na uimarishwaji wa Reli ya kati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here