Meli Kubwa Zaanza KLushusha Shehena Bandari ya Tanga

0

Baada ya kuongeza Kina Cha Bandari ya Tanga kwa kuchoronga Kina Cha Kuingilia Bandarini Hapo Sasa Meli Kuwa Zimeweza Kuingia na Kushusha Shehena Kubwa Jambo lililoshindikana kwa Zaidi ya Miaka 121.

Hapo awali watendaji wa Bandari hiyo walikuw wanalazimisha kukodisha Matishali kutoka Bandari ya Mombasa kupakulia Shehena za Meli kubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shegela ameipongeza Bodi ya TPA chini ya Mkurugenzi Mkuu Deusdedit Kakoko kwa Kupunguza Tozo za mizigo kwenye Bandari hiyo.

“Bandari ya Tanga Ni Miongoni Mwa bandari ambazo imefanyika Kazi nzuri ndio Maana tunaona meli Kubwa yenye Tani 55 imekuja hapa ambapo awali na tozo za zamani usingeona meli kubwa inakuja hapa.” Aliongeza Shegela

Kuboreshaswa kwa Bandari Hiyo kumeleta Fursa Mbalimbali kwa wakazi wa Tanga pamoja na wasafirishaji wanaopeleka mizigo yao kuelekea kaskazini mwa Tanzania ambapo kwa Sasa wanasafirisha shehena kwa Gharama Nafuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here