Meja Kunta na muonekano mpya

0

NA IRENE SABAS, TUDARCO

MSANII maarufu wa singeli Meja Kunta ameamua kubadili muonekano wake kwa kufanya surgery ya meno na kuziba pengo alilokuanalo hapo awali.

Kwa mujibu wa msanii huyo,anaamini kupitia muonekano wake na taswira yake kwa jamii hivi sasa itakuwa ni moja ya njia ya kusogeza kazi zake kwa mashabiki wake.

“Nimeamua kubadilisha muonekano wangu kwasababu hapo mwanzo nilikua na meno yote lakini nilipata ajali ya mgongano ambayo ilisababisha jino kutoka.

“Na baada ya muda kidogo likaanza kuota tena lakini kutokana na umri wa meno kuendelea kuota ulikuwa umepita hivyo basi jino likaishia nusu,” alisema Meja kunta.
Meja kunta, alisema kutokana na hali ya uchumi kuwa ngumu hapo awali ilikuwa vigumu kWake kubadili muonekano wake wa pengo hilo.

“Kutokana na hali kuwa nzuri kwa sasa na naweza kufanya kitu chochote hivyo basi nimeamua kubadilisha muonekano wangu,”lijimwambafai Meja Kunta.

Vilevile Meja Kunta, alisema kuwa alipata wazo hilo baada ya kuona wanafanya na kuamini kuwa inawezekana, pia alipata comments nyingi kutoka kwa mashabiki zake na wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here