Mbunge wa Tanga, atoa mifuko 600 ya saruji kuchangia ujenzi wa madarasa

0

NA MWANDISHI WETU, TANGA

MBUNGE wa Jimbo la Tanga Mjini ambae pia ni Waziri (OMR) Muungano na Mazingira, Ummy Mwalimu, mwishoni mwa wiki amegawa mifuko 600 ya saruji katika Shule tano za Sekondari Jijini Tanga.

Shule hizo ni zile, zinazoendelea na ujenzi wa madarasa ili kuwezesha watoto wote waliofaulu kuanza kidato cha kwanza mwezi huu bila kukosa.

Kwa mujinu wa ofisi ya Mbunge huyo, shule zilizopata mifuko hiyo ya saruji ni pamoja na Shule ya Sekondari Pongwe (Pongwe) na Macechu (Chumbageni).

Nyingine ni Shule ya Sekondari Mikanjuni(Mabawa), Japanri (Tangasisi) na Mnyanjani Kata ya Makorora.

Wakati akikabidhi mifuko hiyo ya saruji, Ummy, aliwataka Wakuu wa Shule na Kamati za Shule kuzingatia miongozo ya Serikali katika kuwachangisha fedha wazazi wa wanafunzi wanaonza kidato cha kwanza.

Alisema kuwa endapo kuna ulazima wa kuchangisha wazazi kwa ajili ya wanafunzi hao ni lazima suala hilo kujadiliwa na kukubaliwa na Wazazi/Walezi wenye watoto katika shule husika.

Aidha, hata wazazi kama itatokea kukubali lakini suala hilo lazima lifike kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kwa maandishi na alikubali au la.

Wakati wakupokea mchango huo wa Mbunge, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahman Shiloow, Madiwani wa kata husika na Mkurugenzi wa Jiji walimshukuru, kwa mchango wake mkubwa katika kuwezesha ujenzi wa madarasa na kuwa wataendelea kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibunge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here