Mbowe, Lema mbaroni kwa kuratibu maandamano

0

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za kuratibu maandamano nchi nzima.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na TBC 1, ambapo ameeleza kuwa licha ya viongozi hao kusema kuwa maandamano hayo ni ya amani, lakini wamebaini uwepo wa vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibufu wa mali za wananchi.

”Tunawashikilia viongozi hao kwakuwa wanahatarisha usalama wa raia na Mali zao kwa kupanga kuandamana nchi nzima kuanzia leo Novemba 02, kwa kuwatumia vijana kuchoma moto miundombinu mbalimbali.” amesema Mambosasa.

Amewataja viongozi wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, Godbless Lema na Boniface Jacob (aliyekuwa Meya wa Ubungo) na Isaya Mwita (aliyekuwa Meya wa Dar es Salaam).

Mapema juzi viongozi wa Vyama vya CHADEMA na ACT- Wazalendo walieleza umma kuwa wameandaa maandamano yatakayofanyika leo nchi nzima kwa lengo la kupinga matokeo ya Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 202.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here