Mbadala wa Mourinho yupo tayari

0

Kocha wa RB Leipzig, Julian Nagelsmann amedaiwa kuwa yupo tayari kujiunga na Tottenham kurithi mikoba ya Jose Mourinho kama timu hiyo itaamua kuachana na Mreno huyo.

Mapema wiki hii The Daily Telegraph iliripoti kuwa Nagelsmann ndiyo chaguo namba moja la mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy ataamua kumtimua kazi Mourinho.

Nagelsmann is the hottest young coaching prospect in the worldWakati Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Leipzig, Markus Krosche amesisitiza kuwa kocha wao Nagelsmann hana sababu ya kutimkia Spurs.

“Julian anajihisi mwenye furaha kuwa hapa, kwasababu kila kitu anachohitaji anapata na maendeleo ya timu ni mazuri. Na ndiyo maana sio sababu ya yeye kuhama hasa ukizingatia bado ana kandarasi na sisi.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here