MATUKIO YA KUKUMBUKWA KATIKA SOKA 2020

0

NA SHEHE SEMTAWA

MWAKA 2020 ambao umefika ukingoni, utabaki ukikumbukwa katika historia ya Afrika na Duniani katika wapenda mchezo wa mpira wa miguu.

Moja ya tukio kubwa la kukumbukwa ni lile la Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kufungiwa miaka mitano na Shirikisho la Soka Dunia (FIFA).

RAIS WA CAF AFUNGIWA MIAKA MITANO NA FIFA

Novemba 23, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ahmad Ahmad, alifungiwa miaka mitano na Shirikisho la soka Duniani (FIFA), kutojihusisha na soka.

Sababu ilielezwa ni matumizi mabaya ya ofisi na pesa za CAF, ambapo Bw. Ahmad alidaiwa kujizawadia pamoja na kujipatia zawadi nyingine kwa jina la CAF.

Ahmad sasa atalazimika kuachia ofisi kabla ya uchaguzi mwezi Machi, 2021, ambapo alikuwa ametangaza nia ya kuwania awamu ya pili.

FIFA kupitia kamati yake ya maadili imeeleza kuwa imefanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha huu ya hilo hivyo mbali na kufungiwa miaka mitano pia amepigwa faini ya shilingi za Tanzania zaidi ya milioni 500.

Rais huyo wa CAF alipigwa marufuku ya miaka mitano na FIFA kwa kukiuka sheria kadhaa za maadili. Makamu huyo wa rais wa FIFA mwenye umri wa miaka 60 alidaiwa kukiuka sheria ya maadili inayohusisha jukumu lake la utiifu, kwa kutoa na kupokea zawadi hatua ambayo ni kinyume na wadhfa wake mbali na matumizi mabaya ya fedha. Taarifa ya FIFA ilisema uchunguzi kuhusu tabia ya Ahmad kutoka mwaka 2017 hadi 2019 ulihusu masuala ya utawala wake katika Shirikisho hilo pamoja na kuandaa na kufadhili safari ya kuhiji Makka ya Umrah, kuhusishwa kwake katika kashfa ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Tactical Steel na shughuli nyengine. Ahmad pia amepigwa faini ya dola za Marekani 200,000.

 

Rais wa Heshima Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ndolanga atoa maoni yake

NOVEMBA 24, Bada ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho hilo la Soka la Duniani, kumuadhibu kwa kumfungia miaka mitano Rais wa CAF, Ahmad Ahmad, Rais wa Heshima Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Muhidin Ndolanga, alisema kitu cha kujifunza katika tukio hilo, kwamba ni lazima kuwafahamu watu wanaotaka kuwa viongozi wa mpira wa miguu Afrika.

Ikumbukwe, Taarifa kutoka FIFA zinaeleza kuwa, kiongozi huyo alifungiwa kujihusisha na mchezo wa soka na shughuli zote zinazohusiana na mchezo huo pendwa duniani, kufuatia kubainika kuwa alikuwa na matumizi mabaya na ufujaji wa fedha za CAF akiwa madarakani.

Kwa mujibu wa Ndolanga kuwafahamu watu hao kutasaidia kupata viongozi waadilifu, waminifu na wanaojiweza  kiuchumi baadala ya kuchagua viongozi wenye dhiki ndogondogo wanaotaka kwenda kuzimalizia kule.

“Unafahamu kwa muda wa siku nyingi nilikuwa sijaingia kwenye mtandao na kutazama huko CAF kuna nini, nimeshtuka jana (juzi), kwamba jamaa amesimamishwa.

“Nilivyoingia kwenye mtandao nikatazama… Nikaona kweli, nikaona kweli…Nikaona oh! Sasa haya mambo mabaya unafaham bwana.

“Kitu ambacho tunajifunaza na katika masuala kama haya ni kwamba ni lazima tuwafahamu watu wanaotaka kuwa viongozi wetu wa mpira wa miguu.

“Lazima tuwafamu vizuri ee… Sio kuwafahamu kwa wasiwassi, tuwafahamu vizuri kwamba hawa watu ni watu barabra, wana uadilifu? Ni waaminifu? Wanajiweza?

“Maana yake haya mambo yanatokea sana kwa sababu mtu ana dhiki ndogondogo hivi nini na nini anataka kuzimalizia kule,”alisema Ndolanga.

Ndolanga, alisema, nafasi ya kuwafahamu watu hao wanayo kwa sababu watu hao wanaotaka kugombea nafasi hizo wanatoka katika nchi zao za Afrika.

“Kwa hiyo lazima tuwafahamu tuwafahamu tusipo wafahamu mapema ndio yanatokea mambo kama haya yanatokea,”alisema Ndolanga.

Akizungumzia kuhusu Tanzania kutajwa katika taarifa hiyo, Ndolanga alisema kuwa hana anachojua kuhusu Tanzania lakini alisikia Cape Verde ndio walipelekewa pesa.

“Ya hapa nyumbani siijui, lakini kama ni kweli hilo nalo ni tatizo kwetu, lakini hilo siwezi nikasema kwa sauti pana, kwa sababu, kwa kusema kweli pengine ni vizuri tukazungumze na wenzetu viongozi wetu wa ngazi ya juu.

“Tukaulize kwamba jamani habari hizi ni kweli ama vipi kwa sababu kama ni kweli litatuletea mgogoro maana yake hawa watu wanapoanza kuwapeleleza watu wa ngazi za juu huwa wanatelemka mpaka chini huku.

“Hawaishii juu wanakwenda mpaka chini kutazama, tazama namna gani mambo yanakuwa vipi… mimi kusema kweli hiyo taarifa inanisumbua sana kwa sababu unajua unaanzaje kumsema ndugu yako yuko hapa na huna uhakika kama amehusika,”alisema Ndolanga.

Ndolanga, alisema ni jambo la kusikitisha kwamba Rais huyo wa CAF alijifikisha katika kuchunguzwa na kukutwa na hatia, kwa kweli ni jambo la kusikitisha.

Muhidin Ndolanga

TFF YATOA UFAFANUZI KARIA KUTAJWA KUPOKEA MGAO

Naye Katibu Mkuu TFF, Wilfred Kidau, alisema taarifa hizo, walianza kuziona kwenye vyombo vya habari vya kimataifa hivi karibuni.

“Na mimi nilikuwa wa kwanza kuona kwenye group ya whatsapp ya makatibu wa Wakuu wa vyama vya mpira wa miguu barani Afrika.

“Na madai hayo yalitaja ‘Tanzanian FA President’ hayakutaja jina lakini sasa nimeona kwenye mitandao yanamtaja ndugu Wallace Karia.

“Kwa hiyo ni habari ambazo tukasema baada ya kuzisoma tuzitolee ufafanuzi.

“Nianze kwa kusema kwamba mwaka 2017 Kamati ya Utendaji ya CAF ilitoa maelekezo kwamba wanachama wake wote wapate dola 100,000.

Katibu Mkuu TFF, Wilfred Kidau

“Na zilikuwa zimeidhinishwa na katika dola 100,000 kulikuwa na mchanganuo wa ni jinsi gani zitatumika kwa maana ya kwamba dola 50,000 zinatakiwa zisaidie program za vijana.

“Dola 30,000 wakati huo, zilikuwa ni kwa ajili ya Waamuzi ambazo kwa sasa hivi CAF wanalipa moja kwa moja na dola 20,000 ni kwa ajili ya marais wa vyama vya mpira wa miguu barani Afrika kwa ajili ya shughuli zao kama marais.

“Hiyo ndio CAF ambapo waliaamua kwa wakati huo, mwaka 2017 wakati wanaamua hayo ilikuwa ni baada Ahmad punde kuingia madarakani ndio aliamua hivyo.

“Kwa hiyo mara ya kwanza Tanzania kupata hela hizo ilikuwa mwaka 2017 kwa maana ya uongozi wa Karia na mimi nikiwa Katibu Mkuu kwa mara ya kwanza tulipata mwaka 2018 na ilikuwa Mei 16 na tulipokea dola 99920 kwa maana ya kwamba ni dola 100,000 kasoro kidogo kutokana na chaji za kibenki na mambo mengine.

“Kwa hiyo niseme kwamba TFF tumepokea fedha hizo mara moja na zote zimeingia kwenye Akaunti ya TFF na kwa maana ya mchanganuo wa matumizi ya zile fedha, Rais wa TFF alipaswa kupata dola 20,000 kwa ajili ya shughuli zake na majukumu ya urais wa TFF,”alisema Kidau.

Kuhusu kushangaa kwake kutajwa jina la Karia katika mgao huo, Kidau, alisema “Ndio maana alivyoona taarifa hiyo aliona ni ya kawaida kwa sababu hazikumtaja jina.

“Lakini nilitaka kutoa ufafanuzi pamoja na kupata zile dola 100,000 kwa maana ya mujibu wa mchanganuo ndugu Wallace Karia alipaswa kupata dola 20,000 lakini ikumbukwe wakati tunaingia kulikuwa na changamoto nyingi za kifedha kutoka FIFA.

“Lakini tulipozipata hizo fedha Rais wa TFF, Karia ziingizwe kwenye matumizi ya kawaida ya TFF ili kuendelea na shughuli zetu za kila siku kwa hiyo hata huo mgao ambao alipaswa kuupata kwa maana ya mchanganuo wa CAF bado yeye hakuupata.

“Tulipata barua wakati huo wa kuelezea hilo jambo, ambayo iliandikwa Mei 2 na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CAF akijaribu kuonesha kwamba mchanganuo wa fedha uko namna hiyo.

“Kwa hiyo, niseme kwamba chochote ambacho kinaongelewa kwenye mitandao ya kijamii ni vitu ambavyo havina ukweli.

“Tuna bahati Watanzania tunaye Leodigar Tenga yeye ni mjumbe wa Kamati ya CAF kwa hiyo wakati wanapitisha hayo maazimio na kuidhinishwa fedha hizo, yeye alikuwa ni miongoni mwa wajumbe walio hudhuria hicho kikao.

“Kwa hiyo kwa namna moja au nyingine tayari tuna mtu ambaye ni shahidi kwamba anajua ni jinsi gani fedha hizo, zinatakiwa kufanyiwa mgawanyo wa aina gani.

“Kwa hiyo mimi ndio Mtendaji Mkuu wa TFF kwa maana ya Acouting Officer wa Taasisi, kwa maana ya fedha zote zinazoingia na kutoka ndani ya Taasisi mimi lazima nijue

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here