Matokeo Kanda ya Ziwa yawashtua Azam FC

0

NA MWANDISHI WETU

KOCHA Msaidizi wa Klabu ya Azam FC, Vivier Bahati, amesema kuwa matokeo ambayo wameyapata kanda ya ziwa kwenye mechi mbili hayakuwa mpango kazi wao hivyo watajipanga kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.

Matajiri hao wa Dar ambao walianza kwa kasi msimu wa 2020/21 kwenye mechi saba za mwanzo walikusanya jumla ya pointi 21 kwa kushinda mechi zote na kujenga ufalme nafasi ya kwanza.

Mambo yamekwenda kombo kwenye mechi zao saba za hivi karibuni ambapo wameshinda mechi moja, sare tatu na kupoteza mechi tatu na kujikusanyia pointi sita walipokuwa wakisaka pointi 21.

Juzi, Desemba 7 ikiwa Uwanja wa Gwambina Complex ililazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC na mchezo wake uliopita Uwanja wa Karume ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United.

Bahati amesema:”Huku kanda ya ziwa mambo yamekuwa tofauti na vile ambavyo tulipanga kwa kukosa kupata matokeo chanya hivyo ni darasa kwetu.

“Bado kuna mechi nyingine mbele yetu hizo tutapambana kupata matokeo chanya ambayo yatatufanya turejee pale ambapo tulikuwa ndani ya uwanja,” .

Mwendo mbovu wa timu uliotesha nyasi kibarua cha Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi Novemba 26 na sasa nafasi yake imechukuliwa na George Lwandamina raia wa Zambia ambaye amesaini dili la mwaka mmoja.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 14 kinara ni Yanga mwenye pointi 34 naye pia amecheza mechi 14 ndani ya Ligi Kuu Bara, msimu wa 2020/21.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here