Mashindano ya mpira wa kikapu kitaifa kufanyika Dodoma

0

NA DOTTO KWILASA, DODOMA

MASHINDANO ya Kitaifa ya ya mpira wa kikapu yanatarajiwa kuanza Novemba 11 hadi 21Mwaka huu jijini Dodoma .

Aidha Mashindano hayo ambapo yatafanyika katika viwanja vipya vya kimakakti vya Chinangali Park kwa kutoa nafasi kwa wadau wa michezo kushuhudia.

Akizungumza na waandishi wa habari hii Jijini Dodoma kuhusiana na mashindano hayo, Mwenyekiti wa Mpira wa kikapu Mkoa wa Dodoma, Michael Kadebe ambaye pia ni kamishna wa mipango na maendeleo wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF), amesema maandalizi ya mashindano  hayo yamekamilika.

Amesema, jumla ya Timu 36 toka Mikoa yote nchini zinatarajiwa kushiriki.

Aidha Kadebe ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo kwenda kuangalia mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Benki ya CRDB.

Licha ya hayo alibainisha kuwa jumla ya shilingi milioni 50 zimetengwa kwa ajili ya vijana wenye umri wa miaka 19 kuonyesha vipaji vyao hasa kwa wale wasiojiweza.

Naye Meneja mahusiano kwa Umma wa CRDB, Godwin Semunyu amesema Benki hiyo imetoa udhamini wa shilingi miilioni 200 za kitanzania huku milioni 50 zikitengwa kwa ajili ya vijana.

” Sisi kama Benki ya CRDB tumeamua kuwanyanyua Vijana ambao wana vipaji vya kucheza Mpira wa kikapu kwa kuwadhamini kutokana na mchezo huo kusahaulika, michezo ina nafasi kubwa ya ajira hivyo wakijiandaa vizuri wanaweza kufikia malengo” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here