Marufuku kuwafungia nyimbo wasanii bila kuwasikiliza

0

Na Mwandishi Wetu

Marufuku kuwafungia nyimbo wasanii bila kuwasikiliza Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Hassan Abbas, ametaka wasanii wasifungiwe hovyo nyimbo na filamu zao bila kushirikishwa.

Badala yake ametaka wasanii hao wawe wanaitwa kwanza na kuelezwa kosa lao kwa kuwa lengo ni kuwasaidia lakini na sio kuwaadhibu.

Dk Abbas aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita Jumatano Desemba 2,2020 alipokutana na wasanii wa filamu na sanaa za maonyesho katika kikao cha mazungumzo kati yao na serikali, kikao ambacho kilihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Dk Kiagho Kilonzo.

Katibu huyo ambaye pia ni msemaji wa serikali, alisema katika serikali hii wasingependa kuona wasanii wakifungiwa hovyo kazi zao bila kushirikishwa. “Wasanii ni watu wakubwa, wasichukuliwe poa ikiwemo kuwafungia hovyo kazi zao bila kuwataarifu, watu wameingia lokesheni wametumia gharama kubwa kuzitengeneza, halafu unaamka asubuhi unaita waandishi unatangaza umeifungia kazi fulani, hii haikubaliki,” alisema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here