Marekebisho ya katiba ya Algeria yapitishwa asilimia 66.8

0

ALGIERS, Algeria 

Marekebisho ya katiba yamepitishwa kwa asilimia 66.8 ya kura zilizopigwa na robo ya wananchi waliojiandikisha kushiriki kwenye zoezi la upigaji kura nchini Algeria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii, Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Uchaguzi ya Algeria Muhammed Shurfi alisema kuwa pingamizi zozote zitakazowasilishwa zitatathminiwa ndani ya siku 10 na matokeo ya mwisho yatakubaliwa.

Kati ya wananchi milioni 23 waliosajiliwa hapo awali, asilimia 23.7 ya wapiga kura pekee ndio iliyoshiriki zoezi la upigaji kura hapo jana kwa ajili ya mabadiliko ya katiba nchini Algeria.

Rasimu ya katiba mpya hairuhusu wagombea wa urais na ubunge kushiriki zaidi ya awamu mbili za uchaguzi mfululizo au kwa nyakati tofauti.

Kwa mujibu wa katiba mpya, Waziri Mkuu ambaye atateuliwa na Rais kuunda serikali nchini Algeria, atalazimika kupata idhini ya theluthi mbili bungeni.

Tofauti na katiba iliyopita, rasimu ya katiba mpya inaruhusu jeshi la Algeria kushiriki katika harakati za kulinda amani za mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Afrika na Jumuiya ya Kiarabu.

Wanajeshi wa Algeria pia watahitaji kuidhinishwa na theluthi mbili bungeni ili kuweza kuhudumu nje ya nchi. Wachambuzi  wanasema kuwa hatua hiyo imeathiri mazingira ya mizozo ya mpakani mwa Algeria na nchi jirani ya Libya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here