Marekani kufunga balozi zake Urusi

0

Marekani inapanga kuzifunga ofisi mbili za ubalozi mdogo nchini Urusi kwa sababu ya masuala ya usalama na ulinzi.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imesema ubalozi mdogo kwenye mji wa Vladivostok na mwingine kwenye mji wa Yekaterinburg ndiyo zitafungwa baada ya mashauriano na balozi wa Marekani nchini Urusi, John Sullivan.

Taarifa ya Wizara hiyo imesema tayari shughuli kwenye ofisi hizo zilikwishapunguzwa tangu mwezi Machi kutokana na janga la virusi vya corona.

Katika miaka ya karibuni mahusiano kati ya Urusi na Marekani yamekuwa magumu kutokana na dhima ya mataifa hayo mawili kwenye mizozo nchini Syria na Ukraine na madai ya Urusi kuwa Marekani inaingilia mambo yake ya ndani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here