MAPOKEZI YA MAGUFULI TANGA USIPIME

0

Na Hafidh Kido, Korogwe

MKOA wa Tanga katika miaka mitano ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli imekuwa na mabadiliko makubwa kiuchumi ikiwemo kufufua viwanda vilivyokufa.

Kutokana na mabadiliko hayo ikiwa ni baada ya kusahauliwa kwa miaka mingi, mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli alisema atahakikisha mkoa huo unarudi katika hadhi yake kama zamani ulivyokuwa ukitegemewa kuzalisha ajira na malighafi.

“Tumejipanga kufanya maajabu. Mkoa wa Tanga ni wa kihistoria tangu enzi za Wajerumani, hata jina shule asili yake ni Tanga kwa sababu shule ya kwanza nchini ilikuwepo Tanga, vilevile ni majiji ya mwanzo Tanganyika.

“Tanga kulikuwa na viwanda vingi vilivyozalisha  ajira, baadaye umaarufu ukaanza kushuka. Ndio mana serikali ya awamu hii tunataka kuifufua Tanga. Hata usafiri wa treni ulikuwa umekufa lakini sasa tumeshafufua treni inatika Tanga kwenda Kilimanjaro hadi Arusha, tunataka mfanye biashara vizuri tunataka gharama za usafiri zipungue,” alisema Dk. Magufuli.

Akizungumzia mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongolenia mkoani Tanga ambalo litakuwa la kwanza duniani kwa urefu kwa mabomba yanayosafirsiah mafuta yenye joto, alisema mradi huo wenye thamani ya Sh  Trilioni 8 liyapita katika mikoa minane na wilaya 24.

Bomba litakuwa na urefu wa kilomita 1,445 huku kati ya hizo kilmita 1,145 zipo upande wa Tanzania. Litazalisha jumla ya ajira 15,000 ambapo Mkoa wa Tanga zipo kilomita 256 zitakazopita katika wilaya tano za Kilindi, Handeni,Korogwe, Muheza na Tanga Mjini.

Aidha, litapita katika Kata 25 na Vijiji 46, huku akibainisha tayari wakazi wa Chongoleani ambao mradi umepita kwenye maeneo yao wameshalipwa zaidi ya Sh Bilioni 3, wengine wataendelea kufanyiwa tathmini huku akiwakumbusha wananchi wa Tanga kuwa mradi huo una fursa nyingi za kiuchumi.

“Nataka kuufanya Mkoa wa Tanga kama kituo cha maendeleo katika ukanda huu, ndiyo maana nawataka ndugu zangu muniletee wabunge na madiwani wa CCM ili waweze kunisaidia. Madiwani wakapange bajeti za halmshauri ili kujua ni namna gani miradi hii inakamilika,” alisema na kusisitiza:

“Maendeleo lazima yapangwe, usipopangwa hakuna kitakachofanyika. Miaka mitano ya mwanzo ilikuwa ya kujipanga, kazi kubwa ilikuwa kujenga uchumi kupitia kudhibiti mapato na matumizi.

“Hawa wanaozungumza mambo ya kukatisha tama hawajawahi kuongoza. Hata kukaa kwa amani na upendo ni kitu kikubwa sana katika taifa.”

Dk. Magufuli aliielezea Wilaya ya Korogwe kuwa miongoni mwa wilaya zilizonufaika na mabadiliko makubwa ya kiuongozi katika miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2015, miradi mikubwa katika sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu na maji imetekelezwa kwa kasi ya kipekee.

“Tumeleta Sh Bilioni 55.7 kwa ajili ya elimu bure Mkoa wa Tanga katika miaka mitano ya awali. Pia tumetumia Sh Bil 17.8 kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ukarabati shule kongwe. Tumejenga shule 228 mpya za sekondari na 905 msingi nchi nzima. Jumla ya Sh Trilioni 1.09 tumetumia kwa elimu bure nchi nzima na Sh Trilioni 2.28 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu,” alisema Dk. Magufuli na kusisitiza:

“Sh Bil 17.4 zimetumika kununua vifaa vya matibabu kwa ajili ya kumaliza tatizo la figo na maradhi mengine Hospitali ya  Bombo. Vilevile tumejenga vituo vya afya 22,  Zahanati mpya tano ambavyo vimesaidia kupunguza umbali wa wananchi kufuata huduma za afya.”

Kukamilika kwa ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za wilaya kumesaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kutokwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bombo na wilaya za jirani kupata huduma ya upasuaji wala X-Ray kwa kuwa huduma zimepelekwa karibu yaomipi Mkumbara, hawaji korogwe.

“Kwenye maji tumetekeleza miradi 64 ambapo miradi 10 kati ya hiyo ipo mjini. Mwana FA (Hamisi Mwinjuma, Mgombea ubunge jimbo la Muheza kwa tiketi ya CCM) tatizo lako la  kusambaziwa maji ni dogo, mradi umefikia asilimia zaidi ya 98 fedha zipo maji yatatoka tu.

“Mkituchagua tena tuna mradi wa kutoa maji Mto Pangani kwa gharama za Sh Bil 200. Ukikamilika utasaidia kuwa na asilimia 95 ya upatikanaji  maji kwa Mkoa wa Tanga,” alisema.

Kuhusu mradi wa umeme, alisema wakati akiingia madarakani mwaka 2015 Mkoa wa Tanga ulikuwa na vijiji 175 vyenye umeme lakini kwa sasa ni vijiji 518 vyenye umeme ambapo  vimebaki vijiji 261 visivyo na umeme mkoa mzima.

Alizungumzia pia ujenzi wa barabara ya Tanga hadi Pangani yenye urefu wa kilomita 50 kwa gharama za Sh Bil 69.8, barabara nyingine ya kutoka Amani hadi Muheza yenye urefu wa kilomita 40.

Vile vile kuna jumla ya kilomita 17.29 barabara za mjini na stendi ya kisasa na mifereji pamoja na dampo la kisasa.

Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM mkoani Tanga, walieleza mambo makubwa yaliyofanywa katika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dk. John Magufuli.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu  alisema kazi kubwa katika sekta ya afya iliyofanya kupunguza vifo vya watoto wachanga na kinamama anaojifungua.

Ummy Mwalimu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here