Mapigano ya Ethiopia yanahatarisha amani nchi za jirani

0

Na Nizar K Visram (Ottawa).

TAREHE 2 Disemba mwaka huu Umoja wa Mataifa (UN) ulitangaza kuwa umefikia makubaliano na serikali ya Ethiopia ili misaada ya kibinadamu iweze kufikishwa jimbo la Tigray lililo kaskazini mwa Ethiopia. Katika jimbo hilo vita vilivyoendelea kwa muda wa mwezi mmoja vimesababisha watu kuuawa na wengine wengi kuyakimbia makazi yao.

Chini ya makubaliano haya UN itaruhusiwa kuingia maeneo ya Tigray yanayodhibitiwa na majeshi ya Ethiopia baada ya kupigana vita dhidi ya chama cha ukombozi wa Tigray (Tigray People’s Liberation Front – TPLF). Misaada ya chakula na madawa itaweza kuwafikia wakimbizi jimboni Tigray na wengine waliovuka mpaka na kuingia Sudan.

Jumla ya wakimbizi laki sita wanahitaji misaada pamoja na wakaazi milioni sita wanaoishi Tigray.

Mpaka sasa serikali ya Ethiopia imekuwa ikizuia misaada hiyo lakini sasa UN imeruhusiwa
Tarehe 4 Novemba Waziri Mkuu wa Ethiopia, Bw Abiy Ahmed aliamrisha majeshi yake
yashambulie vituo vya wapiganaji wa TPLF vilivyo karibu na Mekelle, makao makuu ya Tigray pamoja na uwanja wa ndege wa Humera. Akatangaza hali ya hatari katika jimbo la Tigray. Bunge la Ethiopia ikapitisha azimio la kutangaza kuwa serikali ya Tigray ni batili. Hii ni baada ya Tigray kufanya uchaguzi wake mnamo Septemba baada ya Abiy kuahirisha uchaguzi wa nchi nzima kutokana na Corona.

Bw Abiy Ahmed akatoa muda wa saa 72 kwa wapiganaji kusalimu amri, jambo ambalo lilikataliwa na TPLF. Ndipo njia zote za mawasiliano kama mtandao wa intaneti na simu zikakatwa ndani ya jimbo. Mpaka na Sudan ukafungwa ili kuzuia wapiganaji wa TPLF wasikimbilie huko. Wanahabari wakazuiwa wasiingie Tigray Vita vikaendelea takriban kwa muda wa mwezi mmoja nchini Ethiopia. Majeshi ya Ethiopia inasemekana yalisaidiwa na vikosi kutoka Eritria pamoja na ndege zisizo na rubani (drone) kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Hii ni Ethiopia, nchi yenye watu milioni 110 ikipigana na Tigray yenye watu milioni sita.
Ni Ethiopia ambako kuna makao makuu ya Umoja wa Afrika ambao kauli mbiu yake ni amani barani Afrika.

Bw Abiy alitangaza tarehe 28 Novemba kuwa majeshi yake yameudhibiti mji mkuu wa Tigray, Mekelle. Wiki moja kabla ya hapo aliwaonya wapiganaji wa TPLF kusalimu amri. Walipokataa ndipo akaamrisha majeshi yake yauchukue mji huo. Wakauzingira na kisha kuuteka na kuwafurusha wapiganaji walioingia mitini.
Inaripotiwa kuwa majeshi yalitumia silaha nzito kama vifaru kushambulia mji huu wenye wakazi nusu milioni.

Bw Debretsion Gebremichael, mkuu wa TPLF amesema ilibidi wauachilie mji huo kutokana na utumiaji wa makombora, akitaka UN na Umoja wa Africa waingilie kati na kulaani utumiaji wa silaha nzito dhidi ya raia.

Msemaji wa Abiy amekanusha, akisema si nia ya serikali kuwashambulia raia wake, ingawa
wajumbe wa mashirika ya misaada wamesema wameona raia waliokufa na kujeruhiwa.
Wachambuzi wanasema sasa huenda wapiganaji hao wakaanzisha vita vya misituni na milimani.

Abiy alisema ameamrisha majeshi yake yaingie Tigray baada ya TPLF kushambulia kituo cha majeshi hayo yaliyo katika jimbo hilo. Sababu nyingine ni kuwa TPLF iliendesha uchaguzi na kuchagua serikali ya jimbo kinyume na katiba ya nchi Wachambuzi wanasema katika jeshi la Ethiopia kulikuwa na kutoelewana kwa sababu makamanda wengine hawakuunga mkono mashambulizi ya Tigray. Ndio Abiy akawatengua mkuu wa majeshi,
mkuu wa intelijensia na waziri wa mambo ya nje Ugomvi wa Abiy na TPLF ulianza wakati Abiy alipounda chama kipya cha Prosperity Party badala ya EPRDF kilichoongoza Ethiopia kwa muda mrefu tangu 1991. EPRDF ilikuwa shirikisho la vyama vya majimbo. Vyama hivyo vikatakiwa kuvunjwa na kujiunga na chama kipya cha kitaifa.

TPLF ikakataa kujiunga na chama kipya na ndipo ikaendelea na chama chake jimboni Tigray Chini ya EPRDF chama cha TPLF kilikuwa kinashikilia uongozi wa serikali ya Ethiopia. Kwa kuunda chama kipya Abiy akaamua kuvunja nguvu za Watigray na jambo hili halikukubaliwa na TPLF. Ikaamua kuchagua serikali yake jimboni. Hii ikakataliwa na Abiy kwani aliona inaweza kuchochea majimbo mengine nayo yajitangazie serikali zao
Ndipo Abiy akaamua kutimua wapiganaji wa TPLF kutoka Tigray na nafasi yao kuchukuliwa na majeshi na maofisa wa serikali kutoka nje ya Tigray, hasa kutoka jimbo la Amhara. Matokeo yake ni bendera ya Tigray kuchomolewa na jimbo hilo “kumezwa” na Waamhara. Abiy mwenyewe anatoka kabila hilo. Hii inaweza kuibua hisia kali za kikabila'

Kiongozi wa TPLF, Debretsion Gebremichael, aliliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP);
“Inaelekea Abiy hatuelewi sisi ni nani. Sisi ni watu wenye msimamo imara na tuko tayari kujitoa mhanga ili kulinda haki yetu ya kujitawala”
Tatizo lilianza pale Abiy alipotangaza kuwa anaahirisha uchaguzi mkuu uliokusudiwa mnamo Agosti 2020 kutokana na maambukizi ya Corona. Alifanya hivyo bila ya kusema anaahirisha hadi lini. TPLF ikaona sababu halisi ni kuwa Abiy anaogopa huenda akashindwa na kwa hiyo ameamua kujiongezea muhula bila ya uchaguzi.

Serikali ya Tigray inayoongozwa na TPLF ikaamua kuendelea na uchaguzi jimboni mnamo
Septemba bila ya idhini au kutambuliwa na serikali kuu. Abiy akaona huo ni uasi na akatangaza vita dhidi ya Tigray TPLF iliibuka mwaka 1975 wakati ilipoongoza upinzani dhidi ya serikali ya Mengistu Haile Mariam iliyokuwa ikiungwa mkono na Umoja wa Sovieti (USSR) wakati ule. Mwaka 1991 Mengistu akapinduliwa na muungano wa vyama (Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front – EPRDF). Katika muungano huo TPLF ilikuwa ikiongoza na kwa hiyo uongozi wa nchi ukawa mikononi mwa Watigray wakiongozwa na Meles Zenawi Jimbo la Tigray lina asilimia takriban sita ya raia wote wa Ethiopia. Hata hivyo kwa muda mrefu Watigray wamekuwa wakishika hatamu ya nchi nzima, wakiongozwa na TPLF.

Mfumo huu ulibadilika pale Abiy alipotangazwa rais mwaka 2018. Watigray wakapoteza uongozi na hatamu ikaingia mikononi mwa wananchi wa Oromo ambao ni asilimia 35 wakifuatiwa na kabila la Amhara ambao ni asilimia 27.

Abiy akaleta mageuzi ya kisiasa kwa kuruhusu vyama vya upinzani na kuwafungua wapinzani waliokuwa wamewekwa gerezani. Vyombo vya habari vikapewa uhuru wa kuandika na kusambaza habari. Ili kuleta umoja wa kitaifa Abiy akatengua chama cha EPRDF na kuunda Prosperity Party (PP) bila ya kukubalika na TPLF Vita vya Tigray inaelekea kumalizika kwa muda huu, lakini hii haina maana kuwa amani sasa itatawala nchini. Tigray ilitaka kujitawala ikashindwa lakini mawazo yataendelea – mawazo ya
umajimbo au ukabila. Ni kwa sababu Ethiopia ni nchi yenye makabila mengi yaliyogawanyika kimajimbo.

Ingawa kuna makabila mengi lakini makabila yanayoongoza ni Oromo, Amhara, Somali, Tigray, Sidamo, Gurage, Welaita, Afar, Gambela na Ogaden. Inawezekana baadhi yao yakaanza kudai kujitawala. Tayari kuna Wasomali ambao wamekuwa wakitaka kujiunga na ndugu zao nchini Somalia.

Hivi sasa Abiy ameweka nusu ya majeshi yake jimboni Tigray ili kulinda amani. Amani hii
italindwa kijeshi hadi lini? Kama ikitokezea na jimbo lingine likaanzisha mapigano je ataweza kutuma majeshi huko? Tayari katika jimbo la Oromia kumekuweko na machafuko na maauaji, licha ya kuwa ni jimbo la Abiy mwenyewe.

Ukweli ni kuwa ingawa Abiy Ahmed ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya amani ya Nobel lakini nchini mwake amani inampiga chenga Tukiachia matatizo ya ndani ya Ethiopia kuna pia matatizo ya nchi za jirani ambazo zinaweza kuathirika. Kuna nchi kama Sudan, Somalia, Eritrea na Djibouti ambazo zina historia ya migogoro.

Mataifa makubwa yamekuwa yakijiingiza kijeshi katika maeneo haya kutokana na utajiri wake wa mafuta na madini pamoja na njia ya bahari (Bab al-Mandeb) ambayo inatumika sana kusafirisha mafuta kutoka mashariki ya kati hadi Ulaya. Pia Marekani inajitahidi sana kuzuia China isiingie.

Tigray inapakana na Eritrea ambayo imejinyakulia uhuru kutoka Ethiopia baada ya vita virefu.
Wakati Eritrea inapigania uhuru wake ilisaidiwa na TPLF. Sasa inawezekana Eritrea ikalipa hisani.

Vita vya Tigray vinaweza kuhusisha nchi jirani ya Sudan kwa sababu Watigray zaidi ya 47,000 wamelazimika kuvuka mpaka na kukimbilia Sudan, pamoja na wengine milioni 1.8 ambao wanaweza kuyakimbia makazi yao. Kama mgogoro utaendelea basi huenda idadi hii ikafikia milioni tisa, inaonya UN.

Kwa hivi sasa zaidi ya wakimbizi 800 wanaingia Sudan kila siku. Wote hawa watahitaji misaada ya kibinadamu Sudan nayo imelalamika kuwa Waethiopea laki mbili wamo mbioni wakikimbilia Sudan ambayo itakuwa imeelemewa na wakimbizi. TPLF imemshutumu Abiy kuwa majeshi yake yanatumia ndege za drone alizozipata kutoka UAE ili kuwashambulia Watigray Ndio maana katibu mkuu wa UN Bw António Guterres ametahadharisha kuwa mapigano ya Ethiopia yanahatarisha amani katika nchi za jirani Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu (Amnesty International) limesema tarehe 9 Novemba mamia ya wananchi walishambuliwa na kuuawa karibu na mpaka wa Sudan. Abiy amesema ukatili huo ulitendwa na wafuasi wa TPLF lakini wao walikataa shutuma hizo Naye mkuu wa kitengo cha haki za binadamu katika UN, Bi Michelle Bachelet, alisema hali ya Tigray ni tete na kuna uwezekano wa mauaji yakafika kiwango kikubwa na kugeuka uhalifu wa kivita. Akaongeza kuwa majeshi ya Ethiopia haina haki ya kuwashambulia raia wa Tigray kwa
kudai kuwa wanawaficha wapiganaji wa TPLF

Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye pia ni mwenyekiti wa AU alituma ujumbe wake nchini Ethiopia ili kusuluhisha mgogoro. Hata hivyo serikali ya Abiy ilikataa kuruhusu ujumbe huo kukutana na TPLF.
Abiy alisema: “Ingawa tunapokea ushauri wa marafiki zetu lakini hatutawaruhusu kuingilia mambo yetu ya ndani. Hatutaruhusu ujumbe wowote kuonana au kukaa meza moja na magaidi”

Wakati huohuo Abiy ametangaza kuwa oparesheni ya Tigray imemalizika na majeshi yake
yameliteka jimbo la Tigray. Hata hivyo mkuu wa TPLF Debretsion Gebremichael

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here