Mambo sasa: ‘Tundu Lissu anachokifanya ni kutafuta umaarufu tu’

0

Kamanda wa polisi kanda ya maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHEDEMA, Tundu Lissu ‘anatafuta umaarufu tu’

”Ni kwamba mimi mwenyewe kamanda wa kanda maalumu nilisitisha ule wito, kwa sababu tayari, Inspekta Jenerali wa Polisi alikuwa ameshatoa maelekezo ya kumtaka Lissu akaripoti kule Kilimanjaro”,alisema kamanda Mambosasa.

Tulipokuwa tunamwita yalikuwa mawasiliano kati yetu na Mkoa wa Kilimanjaro, ili ahojiwe kisha maelezo yake tuyapeleke Kilimanjaro lakini baada ya kukuta kwamba afande Inspekta Jenerali wa Polisi ameshamtaka akaripoti kule Kilimanjaro, nikaingilia kati mimi kusitisha wito uliotolewa na mkuu wa upelelezi kanda ya Dar es Salaam.

Kamanda Mambosasa amesema kuwa Tundu Lissu anazo taarifa za kusitishwa kwa wito huo kwa kuwa walikuwa na mawasiliano naye kuanzia siku ya jana.

Hapo jana Tundu Lissu alisema hatatii wito wa polisi kwa kuwa hajui anaitwa kwa makosa yapi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here