Home HABARI Makonda: Mtoto wa mbowe ana corona, Zitto mshirikina

Makonda: Mtoto wa mbowe ana corona, Zitto mshirikina

NA MWANDISHI WETU

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amesema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesitisha mkutano wa kisiasa aliopanga kuufanya baada ya mtoto wake kukutwa na virusi vya corona.

Makonda ameyasema hayo leo Machi 24, wakati alipokuwa Katika ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji hilo yenye mikusanyiko ya watu kuona namna wanavyojikinga na Corona.

Katika ziara hiyo Makonda ametembelea Bandari, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na Kituo vha mabasi ya mikoani vha Ubungo.

“Kama Mbowe asingepata mgonjwa wa Corona angeingiza Taifa hili katika mgogoro mkubwa, Serikali inasema hakuna mikusanyiko yeye anasema tunakusanyika, Mungu katusaidia kutufikishia taarifa ya umuhimu wa ugonjwa huu nyumbani kwake.

“Mngeleta mvutano kati ya serikali na wanasiasa na dunia ingeanza kusema Serikali ya Tanzania haina Demokrasia, kumbe ni wachache wanaotaka kuwatumia wananchi wengi kwa maslahi yao wenyewe.

Aidha katika hatua nyingine Makonda ametoa wito kwa Watanzania kusikiliza ushauri unaotolewa na viongozi wakuu akiwamo Rais na Waziri Mkuu Ili kuchukua tahadhari za kujikinga na Corona na sio kufata maoni ya kila mtu hasa wanasiasa.

“Ukitaka kumsikiliza Rais wako, ukitaka kumsikiliza Waziri Mkuu wako, ukitaka kumsikiliza Waziri wa Afya na timu yake na wataalamu wake kazi kwako, usipotaka kuwasikiliza na ukakubali waganga wakienyeji na washirikina kama kina Zitto Kabwe kazi kwako,” amesema Makonda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -

Most Popular

Yanga yampatia Tshishimbi mkataba mpya

NA MWANDISHI WETU Klabu ya Yanga SC, imesema kuwa tayari imemaliza kazi yake ya kuhakikisha inambakiza kiungo tegemeo wa...

Tetesi za soka barani Ulaya

SANCHO AITIKISA UNITED Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Timu ya Taifa ya Uingereza, Jadon Sancho (20), amesema hatakuwa tayari...

Makonda: Wazururaji hawatakwenda mahabusu watazibua mitaro ya maji machafu

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa watu watakaokamatwa kwenye mkoa huo kutokana...

Chui katika hifadhi ya wanyama ya Bronx akutwa na Virusi vya Corona

NEW YORK, MAREKANI Chui wa kike wa Malaysia aliyefahamika kwa jina la Nadia mwenye umri wa miaka minne katika hifadhi...

Recent Comments