Majukumu yetu yatagusa maisha ya wananchi- Ummy

0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu  amesema atahakikisha utekelezaji wa majukumu ya kusimamia masuala ya Muungano na Mazingira yanagusa Maisha ya wananchi moja kwa moja kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumza na Menejimenti ya Ofisi yake mara baada kupokelewa rasmi katika Ofisi za Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma Jana, Mwalimu amewataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo chanya kwa taifa.

“Tuna jukumu kubwa la kulinda na kuhifadhi mazingira pamoja na kudumisha muungano wetu ambao ni tunu ya Taifa letu” amesisitiza Ummy.

Amesema ni muhimu kuendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa Muungano kwa kushirikisha vijana ambao ni taifa na leo, hususan waliozaliwa baada ya muungano kwakuwa kuna mengi ya kujifunza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here