Majaliwa alitaja zao la chikichi kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati

0

Na Merciful Munuo,Kigoma

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa amelitaja zao la Chikichi kuwa miongoni mwa mazao 7 ya kimkakati, ambayo serikali imewekeza nguvu zake katika kuinua na kuimarisha kilimo chake hapa nchini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati wa mkutano na wadau wa sekta ya kilimo mkoani Kigoma ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi imeamua kuwekeza kwenye zao la Mchikichi, kutokana na uhitaji wa mafuta ya maweze ambayo nchi pia imekuwa ikiagiza nnje ya nchi.

“Haiwezekani tuwe tuna mashamba ya kutosha, na yenye rutuba vizuri halafu tushindwe na majirani zetu ambao hawana ardhi kubwa kama ya kwetu” aliongeza Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa aliyataja mazao mengine ya mkakati kuwa ni pamoja na Tumbaku, Chai, Kahawa, Pamba, Katani (Mkonge), zao la Chikichi pamoja na Korosho.

Waziri mkuu Majaliwa pia amezitaka taasisi za kibenki kutoa mikopo yenye riba nafuu na kuhakikisha kuwa wakati wa kurejesha mikopo hiyo unaendanana na wakati wa kuvuna kwa mikopo ya wakulima ili kutowakwamisha kwenye urudishaji wa madeni yao ili waweze kuwekeza kwenye mazao ya kimkakati ikiwemo zao la chikichi.

“Hili suala la mikopo muangalie muwe na vifurushi vya walahu miaka mitatu kwa wakulima hawa maana hauwezi kumpa mkulima kifurushi cha miezi 6 halafu yeye anategemea kuvuna baada ya miaka mitatu utamdai tu ” alielezea Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri mkuu alieleza kuwa mazao haya ya kimkakati, ikiwa yatapewa kipaumbele yatasaidia kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na nchi kwa ujumla kwani uhitaji wa mazao haya ni mkubwa duniani.

Waziri mkuu Majaliwa pia amemuagiza waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda kutafuta wawekezaji wa kilimo cha zao la chikichi pamoja na kutoa mashamba kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye kilimo cha zao hilo.

Vilevile kassim majaliwa wakati akijibu maswali ya wadau wa sekta hiyo wakiwemo wakulima walikuwa wakijadili hoja mbalimbali, pia ameagiza tafiti kufanyika ili kubaini ikiwa kuna ugonjwa umeingilia zao hilo pamoja na kutafuta maeneo yenye ardhi yenye rutuba kwaajili ya kilimo chake.

Zao la chikichi limekuwa miongoni mwa mazao muhimu duniani, kutokana na uzalishaji wa mafuta ya m,aweze ambayo yamekuwa yakitumika kama mafuta ya kupikia pamoja na tiba.

Kwa mujibu wa rekodi za mtandao wa wikipedia nchi zinazoongoza zaidi kwa kilimo cha michikichi ni pamoja na nchi za Malaysia na Indonesia zenye mavuno ya 80% ya mawese duniani, huku nchi za Brazil na Kolumbia zikiwa ziemanza vilevile kupanda Michikichi kwa wingi.

Uwekezaji katika Kilimo cha zao la Mchikichi fursa iliyotajwa kusahaulika mkoani Kigoma
Michikichi ni zao mojawapo ya mazao ya mafuta ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Kigoma, Mbeya na Tanga hapa nchini Tanzania.

Aidha zao hili hulimwa pia kwa kiasi kidogo katika mikoa ya Kagera, Pwani, Rukwa, Morogoro na visiwa vya Pemba na Unguja. Mkoa wa Kigoma ukiwa ni eneo muhimu kwa uzalishaji wa zao la michikichi hapa Tanzania kwa mwaka huzalisha zaidi ya tani 2,000 za mawese na zaidi ya tani 450 za mafuta ya mise.

Zao la mchikichi limekuwa mkombozi kwa wakulima wengi wa Mkoa wa Kigoma kwani hutumika kwa chakula, biashara, mafuta ya mise hutumika katika mapishi ya vyakula mbalimbali pia husaidia mwili kupata nguvu na joto na hutumika katika utengenezaji wa sabuni na vipodozi mbalimbali.

Hata hivyo nchi za Indonesia na Malaysia ambazo zilitoa mbegu ya zao la mchickichi kutoka Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania miaka ya 1960 kwa sasa zinaongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa mafuta ya mawese na bidhaa zitokanazo na michikichi.

Malysia pekee huzalisha tani milioni 18.79 million za mafuta ya mawese na kusambaza tani milion 18 za mazao yanayotokana na zao la michikichi duniani yakiwemo mafuta ya mawese ambayo Tanzania imekuwa ikiagiza takribani asilimia 65 ya mafuta ya mawese kutoka nchini ya Malaysia, zikifuatiwa na nchi nyingine kama Kolumbia na Thailand.

Kwa ukanda wa Afrika nchi za Nigeria, Kenya, Ghana, Cameroon na Benin zinatajwa kuongoza katika uzalishaji wa zao la mchikichi ambapo nchi ya Naigeria huzalisha tani milioni 2.3 ya mafuta ya mawese kwa mwaka na kuifanya kuwa nchi ya tatu kwa uzalichaji kidunia.

Kiasi hiki ni kingi ukilinganisha na fursa na uaptikanaji wa zao hili nchini Tanzania hususan Mkoa wa Kigoma haipo katika rekodi ya uzalishaji. Sababu kubwa zinazofanya zao hili kutojulikana na hata kutomnufaisha mkulima wa kawaida nchini Tanzania ni teknolojia duni ya kilimo cha zao hili na ukosefu wa miunndombinu ya kuchakata mazao yatokanayo ya mchikichi hususan viwanda.

Kwa upande mwingine wataalamu wa kilimo hawajaweza kutilia maanana juu ya umuhimu wa zao hili, Serikali nayo haijawea kipaumbele namna ya kutoa ruzuku kwa wakulima wa zao la mchikichi ili waweze kujikwamua kiuchumi,

Kadhalika bidhaa mathalani vile mapaa ya ndani (ruffing Materials) ambayo hutokana na makapi ya mchikichi huingizwa kwa wingi nchini kutoka Malaysia, na Afrika ya Kusini. Wakulima wa zao hili wengi hutumia zana duni katika kuchakata mazao ya michikichi kiasi ambacho hakiwapi tija kukuza uchumi.

Sambamba na ukosefu wa zana za kilimo nguvu ya serikali kupitia wizara ya Kilimo ingeweza kufikiri namna ya kuwashirikisha wadau wa maendeleo, mashirika binafsi ili kushawishi uwekezaji katika zao la mchikichi kwa Kuweka miundombinu kama nishati ya umeme kwaajili ya kujenga viwanda.

Kwakuwa zao hili hutoa malighafi zaidi ya tatu ingekuwa fursa kwa wakulima kutengeneza wigo wa upatikanaji wa biashara za mazao ya mchikichi kama vile vipodozi, vyakula vya mifugo, sabuni na mafuta ya kupikia na bidhaa nyingine nyingi kadha wa kadha.

Serikali kwa kutumia wataalamu wake katika ngazi mbalimbali ikiwemo Halmashauri, na ngazi mbalimbali za uongozi hazina budi kushirikiana na mashirika mbalimbali ya maendeleo katika kuhakikisha kuwa zao la michikichi linakuwa moja ya mazao makuu katika kukuza kipato na kuwaondolea umaskini wananchi wa mkoa wa Kigoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here