Majaliwa aeleza mazao ya bustani yalivyosaidia kukabiliana na Corona Tanzania

0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mazao ya bustani nchini yalisaidia Watanzania kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa corona akibainisha kuwa kuna umuhimu wa kuwekeza zaidi katika fursa za soko la mazao hayo duniani.

Akizungumza leo Jumamosi Desemba 5, 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la kikanda kuhusu uwekezaji na biashara ya mazao ya bustani, Majaliwa amesema dawa mbadala za asili zilizosaidia wananchi duniani kote kudhibiti ugonjwa huo zilitokana na sekta  ya bustani.

“Mazao ya bustani yamekuwa msaada katika kupambana na ugonjwa hatari wa corona. Wote ni mashahidi mahali ambapo kulikuwa na msisitizo wa ulaji wa mazao ya mboga mboga, viungo na matunda na imetusaidia sana.”

“Kutokana na vielelezo hivyo ni wazi mchango wa kilimo cha bustani kwenye maendeleo ya watu, uchumi na dunia kwa ujumla ni mkubwa na iwapo fursa hizi zikifanyiwa kazi zaidi basi safari yetu ya kuelekea uchumi imara zaidi itakuwa na mafanikio makubwa,” amesema Majaliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here