Magufuli atuma salamu vifo 15 ajali Kagera

0

NA MWANDISHI WETU

Rais Dk. John Magufuli amepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya watu 15 vilivyosababishwa na ajali ya barabarani baada ya basi la abiria kupinduka katika mteremko wa Kumnyange uliopo katika Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.

Ajali hiyo ambayo ilitokea jana ilisababisha majeruhi ya watu 18 ambapo Rais Magufuli alimtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brig. Jen. Marco Gaguti, na amemtaka kufikisha salamu za pole kwa familia za marehemu, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo.

Aidha Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wa[pone haraka na kuungana na familia zao.

“Nimesikitishwa na vifo vya Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii nawpa pole wafiwa wote nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi,” alisema Rais Magufuli katika taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumiaji wote wa barabara hasa madereva wa magari kuzingatia sheria zote za usalama barabarani ili kuepuka jail zinazoweza kuzuilika.

Aidha amevitaka vyombo vinavyosimamia usalama barabarani kuchukua hatua dhidi ya watumiaji barabara wanaokiuka Sheria za uslama barabarani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here