Magufuli atangazwa mshindi kiti cha urais

0

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza mgombea wa CCM, John Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya kupata kura 12,516,251 akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Tundu Lissu aliyepata kura 1,933,271.

Aidha katika matokeo hayo Bernard Membe wa ACT Wazalendo amepata kura 81, 129.

Akizungumza katika kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mst. Semistocles Kaijage amesema mgombea huyo amepata kura nyingi halali kuliko mgombea mwingine yeyote.

“Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ilikuwa 29,754,699, idadi ya waliopiga kura ni 15,09,950, Kura halali ni 14,83195 na kura zilizokataliwa ni 261,755,” amesema Jaji Kaijage na kuongeza kuwa

“Kufuatia ushindi wa Dk. Magufuli, namtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania kupitia CCM.”

Katika Hatua nyingine Jaji Kaijage amesema wateule hao watakabidhiwa hati za ushindi Jumapili Novemba Mosi, 2020.

Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here